Home -- Kiswahili -- 01. Conversation -- 1 Great Commission
01. Mazungumzo na Waislamu kuhusu Kristo
1 - Agizo La Utume Mkuu Wa Yesu Bwana Wetu
Kwa nini Wakristo wanapaswa kushiriki imani yao na Waislamu? Kuchunguza agizo kuu la Yesu kwa wanafunzi wake, lililo katika Mathayo 28:19-20, kunatoa mwanga kuhusu sababu na namna huduma hii inavyopaswa kutekelezwa. Hapa, agizo kuu la Kristo linawekwa kulinganisha na amri za Muhammad kwa wafuasi wake za kueneza Uislamu.
1.01 -- Kichwa
1.02 -- Wito
1.03 -- Mamlaka yote mbinguni na duniani
1.04 -- Kwa sababu hiyo: nendeni!
1.05 -- Uongozi wa Roho
1.06 -- Tunayo nini ya kutoa?
1.07 -- Kwa Watu wote
1.08 -- Agizo na utume mkuu upande wa Uislamu
1.09 -- Amri ya ubatizo katika Utatu Utakatifu
1.10 -- Ubatizo unaleta ulinzi na usalama
1.11 -- Ubatizo – kiunganisho kuingia katika nguvu za Mungu
1.12 -- Kutii maagizo ya Kristo
1.13 -- Tendeni yote niliyowaamuru!
1.14 -- Lengo ya amri (maagizo) ya Kristo ni nini?
1.15 -- Sheria ya Mhammad
1.16 -- Kusudi la siri baina ya sheria ya Mhammad na ya Yesu
1.17 -- Mimi nipo pamoja nanyi!
1.18 -- Hadi mwisho wa ulimwengu wote
1.19 -- Hadi mwisho wa dahari!
1.20 -- Je, Allah yu pamoja na Waislamu wake?
1.21 -- Nene “wote” lipo mara nne katika Agizo la utume mkuu
1.22 -- MASWALI
1.01 -- Agizo La Utume Mkuu Wa Yesu Bwana Wetu - Jibu la Waislamu
“Nao Walipomwona, walimsujudia; lakini baadhi yao waliona shaka. Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia, Nime pewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari. Amina.“
(Mathayo 28:17-20)
1.02 -- Wito
Baada ya Yule, aliyekuwa amesulibiwa na kufufuliwa, naye alipoukamilisha upatanisho wa ulimwengu na Mungu, alitaka kutoa wokovu wake kwa kila mtu wa mahali pote kwa njia ya wanafunzi wake. Kwa kujitoa kafara kwa ajili ya dhambi za wanadamu wote, yeye mshindi juu ya kifo na kuzimu aliwaita wale waliomwabudu na wafuasi wake, ambao bado walikuwa na mashaka, akawaamuru kutangaza wokovu wake kwa mataifa yote. Wanafunzi wake wote walitoroka saa ya kujaribiwa kwake. Hakuna kati yao aliyestahili kuamriwa kuwa mtumishi wa Kristo aliye hai. Wito wake tu uliwafanya kustahili kuwa wajumbe wa neema yake.
1.03 -- Mamlaka yote mbinguni na duniani
Kristo aliwafunlia wafuasi wake kwamba, Baba yake wa mbinguni amempatia mamlaka yote juu ya malaika na juu ya binadamu wote, juu ya sayari zote za angani na kila nguvu kani yote duniani. (Ufunuo 5:1-14).
Jinsi gani Mwenye Enzi alithubutu kukabidhi enzi yake yote kwa Mwana wake? Hakuweza kuhofia ghasia, au maasi dhidi yake? Baba alikuwa anamjua Mwana wake. Alikuwa ni myenyekevu na mwadilifu moyoni. Hakuthubutu kujifanya kuwa mkubwa. Alijitoa kuwa dhabihu yeye mwenyewe kwa ajili ya watenda dhambi wasiostahili. Daima alimheshimu Baba yake kwa namna ambavyo Roho Mtakatifu kila wakati pia anamtukuza Mwana. Mungu wetu ndiye Mungu Mnyenyekevu. Kwa sababu hizo Baba aliweza kukabidhi enzi zote za mbinguni na duniani kwa Mwana wake.
Roho tofauti kabisa inatawala Uislamu. Qur„ani inatueleza kwamba haiwezekani kuwa na miungu wawili, kwa sababu kwa uhakika mmoja angeinuka dhidi ya mwingine (Sura al-Mu„minum 23:91). Wakati wa enzi za Ottomani baada ya kifo cha Sultani fulani wana wake wote, isipokuwa yule mmoja mwerevu na mwenye nguvu, waliuawa wote, ili kuzuia mapigano kuhusu urithi wa kiti cha enzi. Roho ya maasi inatawala ndani ya Uislamu, maana hata jina moja kati ya majina 99 la Allah linalopendeza sana ni “Mwenye kiburi, na mwenye majivuno” (Sura al-Hashr 59:23).
Upande wa Yesu hali ni kinyume cha hayo. Yeye hakutumia mamlaka yake kujenga utawala wa kidunia kwa kukusanya kodi na maaskari. Badala yake aliwaponya wagonjwa wote waliomjia, aliwafukuza mapepo wachafu kutoka kwa wale waliopagawa, aliwafufua wafu, alisamehe madhambi na aliwamiminia Roho Mtakatifu wanafunzi wake waliomngojea kwa maombi. Alianza kujenga utawala wa kiroho na kuonyesha mamlaka yake kwa kuwafanya wapya wanafunzi wake. Jina lake “Yesu” ndio pekee and inabaki katika malengo ya maana halisi ya jina lenyewe: “Ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao” (Mathayo 1:21).
1.04 -- Kwa sababu hiyo: nendeni!
Baada ya Yesu kupokea mamlaka yote kutoka kwa Mwenyezi, aliwaagiza wanafunzi wake wainuke na waanze kwenda. Huku wakitegemea nguvu yake isiyokoma, waache kujificha na kujaribu njia mpya. Yesu hutufundisha namna ya kutembea na kuharakisha! Anatutaka tuache kumezwa kabisa na mambo binafsi. Anajaribu kutuweka huru kabisa na “Umimi” wetu na kutuelekeza kwa wenzetu, yaani “Wewe”. Anatutuma kwa jamaa na jirani. Na zaidi anatutaka tuvuke makundi na mashirika yetu ya karibu nasi, ndipo tumuige yeye Mchungaji Mwema aliyewaacha wale 99 waliojisikia kuwa wenye haki, akaenda kumtafuta yule kondoo mmoja aliyepotea mpaka ampate (Luka 15:4-7).
1.05 -- Uongozi wa Roho
Yeyote atakayetii agizo la Yesu, atahitaji sana kuongozwa kiroho. Labda utasema: “Nitaenda kwa nani? Sina anuani zao!“ Bwana anakujibu”: “Omba nawe utapewa!” (Mathayo 7:7; Luka 11:9-13; Marko 11:24). Tunayo nafasi ya kumuomba atupe uhusiano na Waislamu wanaomtafuta, ambao mioyo yao na nia zao zimetayarishwa na Roho Mtakatifu.
Naye atakayemwona mtu wa namna hii, basi asimsemeshe kabla ya kugundua anayowaza na ajisikiavyo, na anasumbuka na nini. Hata baada ya hapo asimtolee majibu aliyotayarisha mwenyewe, bali amwulize kwanza Yesu moyoni, ni jambo gani ambalo yeye anahitaji kumwambia mtu huyu. Twaweza kuuliza maneno ya kufaa kwa wakati wake na kwa mtu aliye wazi; hata hivyo, Yesu anapotuambia namna ya kutamka, basi tusinyamaze, bali tumwambie wazi na mengine tumwachie Yesu ni jinsi gani neno lake litakavyofanya kazi kwa njia yetu ndani ya yule mtu amtafutaye.
Jipime mwenyewe! Je, unasikia wito moyoni useme na jirani yako, mfanya kazi mwenzako, mke wako,watoto wako au mtu yeyote mwingine habari za Yesu? Chunguza pamoja na Yesu kwa njia ya maombi habari ya mapenzi yake na agizo lake kwako. Usisite kuwa mtiifu kwake. Na ukijisikia kuzuiwa au kuwa mwoga, basi umuombe Yesu akujalie upendo wake na nguvu ya kwamba, uweze kushinda mazuia hayo ya ndani yako! Wako watu wengi zaidi kuliko unavyoona wanangojea ushuhuda wako unaoongo zwa na Roho! Hata hivyo, sala zako zinazotangulia zina umu himu kuliko hata ushuhuda wenyewe.
1.06 -- Tunayo nini ya kutoa?
Yeyote atakaye usikivu kwa rafiki zake, basi na atoe kwao yale ambayo wanayatafuta wao, hata bila kuweza kutamka wao wenyewe. Mwalimu bora anajua zaidi kuliko wanafunzi wake, akiweza kufanya yale, ambayo wao hawawezi; bado wanatamani kufahamu na kutenda sawa na yeye. Hawamtazamii mwalimu wao awashurutishe kwa maneno makuu, bali waone kama mwalimu wao anayo uwezo na mambo hasa ya kiroho, na kama anaishi sawasawa na mafundisho yake. Kama ni hivyo, watamsikiliza na kuchangamana naye wakimzunguka kwa hamu. Ndivyo ulivyo ualimu bora.
Wakristo wanalo jambo la kutoa kwa wale walio nje ya imani yao, ambalo wao hawana. Wakristo wanafahamu kwamba, Mungu ndiye Baba yao, Yesu ni Mwokozi wao na Roho Mtakatifu ndiye Mfariji wao. Yeye anatupa haki kwa njia ya neema tu. Naye anatujalia Roho wake mwenyewe kama zawadi. Yeye huumba amani ndani yetu na furaha isiyokoma. Alimimina upendo wake kwa kujitoa kabisa ndani yetu (Warumi 5:5) naye alitujalia kujua kusudi kuu ya maisha yetu. Alifunua ukweli wake wa milele kwa wafuasi wake (Yohana14:6) na kuwapa tumaini kwa ajili ya siku zijazo. Alitugusa kwa mamlaka yake isiyokoma. Inatupasa kusahau hali yetu ya chini, masumbuko yetu mengi, na tuanze kushuhudia kwa maombi yale, ambayo Bwana wetu aliyefufuka ametutendea kwa neema yake. Tunatakiwa kutoa kwa ajili ya ulimwengu jambo, ambalo ulimwengu unalitafuta. Wafuasi wa Kristo wamepokea uzima wa milele kutoka kwa Mwana Kondoo wa Mungu. Basi uwashirikishe jamaa na majirani zako makuu haya!
1.07 -- Kwa Watu wote
Agizo kuu la Yesu iliumba mwendo wa misheni usiokoma katika miaka hii 2000 iliyopita.Wajumbe wake kwanza walipeleka Injili katika nchi zinazozunguka Bahari ya Kati na nchi ya Uajemi. Ndipo wokovu ukaelekea Ulaya na Asia ya Kati hadi ndani ya Uchina. Pamoja na uvumbuzi wa Marekani na njia ya baharini kusafiri hadi India, Bwana wetu aliyefufuka akafungua nchi zote duniani kwa ajili ya mashahidi wake. Siku hizi watoto wa Ibrahimu, Wayahudi na Waislamu wanakabiliwa na uamuzi wa wamwamini Yesu au kumkataa. Hata nchi za kikomunisti, kama vile Urusi uliogawanyika sasa na Uchina pia Injili imepenya ndani. Hata hivyo tusisahau kwamba, hadi sasa ni sehemu ya tatu tu ya wanadamu wote wanajiita Wakristo. Sehemu kubwa zaidi ya wakazi wa dunia hii hawamjui Mwokozi wao. Bado kuna mengi ya kufanya. Hatuwezi kujikalia tu na kupumzika. Kila mwanafunzi wa Yesu mmoja-mmoja anaitwa kuchangia sehemu yake kwa ajili ya kufikia wanadamu wote!
1.08 -- Agizo na utume mkuu upande wa Uislamu
Ukristo sio dini pekee yenye nguvu ya kuenea katika ulimwengu wote. Qur„ani nayo inaagiza mara mbili:
"Uwapige (kwa silaha) hadi kukomesha jaribu (la kupinga Uislamu) lisisalie tena na dini ya Allah ibaki peke yake...” (Sura al-Anfal 8:39; al-Baquara 2:193).
Zaidi ya aya100 ndani ya Qur„ani zinachochea Waislamu washiriki katika vita vitakatifu (jihad). Tunaweza kusoma: “Kwa kweli, Allah alinunua roho na mali ya waumini, ili wapate kufikia paradiso. Wanapigana vita kwa ajili ya njia ya Allah, hivyo wataua na kuuawa” (Sura al-Tawba 9:111).
Bahati mbaya, Wakristo nao walianzisha vita vya ki-dini na kuteka nchi kadhaa (ki-koloni) kwa manowari. Basi matendo hayo ya kuasi sheria, yalikuwa kinyume ya agizo la Yesu Kristo, aliyemwambia Petro: “Rudisha upanga wako mahali pake, kwa sababu yeyote atumiaye upanga ataondolewa kwa upanga” (Mathayo 26:52)
Uislamu ulienea kupitia mawimbi mawili makubwa: Shambulio la kwanza lilidumu kwa miaka 100 na kuzishinda nchi za Kati za Karibu, Afrika ya Kaskazini, Uispania, Uajemi na sehemu za Asia ya Kati.
Wimbi la pili lilikuja na watu wa Mongolia na mateka yao. Wengi wa watoto wa Genghis Khan walipokea Uislamu kama sababu za kidini kwa ajili ya kuhalalisha mapigano yao. Waliikandamiza Asia ya Kati na wakaja kutawala Uchina, India ya Kaskazini, Mesopotamia na Urusi. Waturki wa Ottoman, waliokuwa jamaa zao, walishinda jiji la Konstantinopeli mwaka 1453 na walitaka kuiteka Vienna mara mbili bila kufaulu. Vurugu na mavutano katika maeneo ya Balkani (kaskazini ya Ugriki) na sehemu za Mashariki ya Karibu ni shida nyingi katika eneo hili ni madai yasiyoweza kusuluhiswa kutokana na utawala wa Ottoman wa miaka 400.
Wimbi lingine la tatu la kupanuka kwa Uislamu lilianza 1973 kwa kupanda kwa bei ya mafuta ya ardhini, na hilo limeendelea kupitia bara zote za dunia. Kabla ya hapo hawakuwahi kuishi Waislamu wengi hivi katika nchi za Matengenezo ya Dini (Reformation) kama leo! Je, muda gani tena Wakristo wanataka kulala na kuona ndoto yao ya kushiriki katika jamii iliyochan ganyika kwa mapokeo mbalimbali kama ilivyo sasa?
Baadhi ya Waislamu wanaosisitiza kwamba Uislamu dini ya maridhiano na ya amani (tolerant), na ni dini ya kupenda amani. Makumi ya aya ndani ya Qur„ani inawahimiza kwa ustahi wa tabia na kushindana katika matendo mema tu (Sura al-Baqara 2:256; al-Ma„ida 5:47; al-Ankabut 29:46 na penginepo) Kweli, aya kama hizi zinapatikana ndani ya Qur„ani, lakini zilitungwa wakati Mhammad na wafuasi wake bado walikuwa wachache. Matamshi hayo ya kutaka kuchukuliana kwa amani baada ya hapo yalitanguliwa kihalali kwa maagizo kadhaa ya Allah katika Qur„ani; pamoja na hayo aya hizo zingine zinawaita Waislamu kwenye vita vya silaha, kusudi kutisha maadui wote (Sura al Baqara 2:191; al-Tawba 9:28 na penginepo). Kwa Mjibu wa Sharia maneno hayo ya awali ya kuchukuliana hadi leo yamepitwa na yameshatanguliwa na sio halali tena. Hata hivyo, aya hizi zilizotanguliwa bado zinanatumika na kukazwa sana na Waislamu wanaoishi kipekee nje ya uma wa Kiislamu. Mhammad mwenyewe alitamka mara kwa mara: Vita ni udanga nyifu! Dunia ya uenezi wa Uislamu haikujengwa kwenye ukweli, bali kwenye hila. Allah mwenyewe ndiye mwenye hila kuu kuliko wote (Sura Al Imran 3:54; al-Anfal 8:30)!
1.09 -- Amri ya ubatizo katika Utatu Utakatifu
Yesu hakufundisha taratibu za mashaka juu ya Mungu. Hakumfunua Allah asiyetambulikana, mkubwa na ailye mbali mno! Mwana wa Mungu alifunua jina la Baba yake mara 187 ndani ya injili zote nne na alitujalia Roho Mtakatifu wake, aliye pia Mungu Kweli. Yesu naye alikiri: “Mimi na Baba tu Mmoja (- sio wawili)!” (Yohana 10:30; 17:21-22). Aliwaagiza wanafunzi wake kuwabatiza wote waaminio ujumbe wa injili; na sio katika majina ya miungu watatu mbalimbali, bali katika la jina lile moja la Mungu, aliye Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Hao watatu ni umoja kamili, jinsi Yesu alivyosema: “Baba ni ndani yangu na mimi ni ndani ya Baba” (Yohana 14:10-11).
Kufuatana na wafafanuzi mbalimbali wa Qur„ani, kimaajabu Mhammad anataja ubatizo ya Wakristo na anauita: “ni sura yao (au rangi yao)” (al-sibghat). Alielewa kwamba, Wakristo walikuwa tofauti na watu wengine kwenye mkondo wa nchi za Arabuni. Wao hawakuiba, hawakuringa, kila mmojawao alikuwa na mke mmoja tu, walikuwa watu wapole na hata wakiwapenda maadui zao (Sura Al Imran 3:55, 199; al-Ma„ida 5:66,82; al-An„am6:90; Yunis 10:94; al-Nahl 16:34; al-Hadid 57:27; al-Saff 61:14 na penginepo). Alihesabia sifa hizo kuwa ni uamsho wa kiroho kutokana na ubatizo wao, mwongozo wa injili na agano lao nzito walio nao na Mungu (Sura al-Ma„ida 5:110; Maryam 19:88; al Ahzab33:7).
Hata hivyo, Mhamadi aliingia kwenye mabishano makali dhidi ya uungu wa Kristo na uungu wa Roho Mtakatifu. Ukiri hasi wa kukanusha uliojumuika mara mbili katika shahada inayosema: “Hakuna mungu ila Allah!” Hivyo agizo la Yesu la kubatiza watu katika jina la Mungu Baba, Mwana na Roho Mtakatifu linasikika kama kumtukana Mungu katika masikio ya Waislamu. Kwa vile katika Uislamu hakuna Roho Mtakatifu jinsi ilivyo katika Injili, basi haiwezekani kuwa na utambulisho wa Baba, Mwana na Roho Mtakatifu ndani ya Waislamu (1.Wakorintho 12:3; Warumi 8:15-16).
1.10 -- Ubatizo unaleta ulinzi na usalama
Paulo anaandika: “Neema ya Bwana Yesu Kristo, na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.” (2.Wakorintho 13:14) Ubatizo unatupatia uhusiano binafsi na Mungu na ulinzi wa ndani ya Utatu Mtakatifu. Tumeunganishwa ndani ya Baba, Mwana na Roho Mtakatifu kwa njia ya ubatizo wetu. Mungu mwenyewe ndiye ngao yetu. Mtu adumuye katika upendo, basi anadumu ndani ya Mungu na Mungu ndani yake. Inatupasa kuvaa silaha zote za Mungu na hivyo kuwa wenye nguvu “ndani”ya Bwana, ndipo yule mwovu hawezi kupata nguvu ndani yetu (1.Yohana 4:16; Waefeso 6:10-17 na penginepo).
Mambo ya siri za ndani ya Uislamu hazitoshelezi na taratibu za kufikiri tu juu ya Allah katika dini yao, na wanatetemeka kwa ajili ya sheria za Allah juu ya kila mtu na hali yake ya baadaye, iliyo ya sehemu mbili (kwenda paradiso au kwenda jehanam). Wanajaribu kwa kutafakari sana kumfikia Allah, aliye mbali, mwenye enzi yote na asiyefikika. Wanajaribu kupenya ndani yake au kumgeuza, ili kusudi wampate awe anaishi ndani ya miili yao. Mara nyingi wanapagawa chini ya nguvu ya roho chafu kwa njia ya mazoea ya uganga au uchawi. Allah ndani ya Uislamu hafikiki na asiyefahamika, kwa hiyo aina zote za ushirikina zinaweza kuwaambukiza Waislamu kwa urahis sana. Pia hakuna wokovu ndani ya Uislamu. Kuna wito halisi tu wa kujiweka chini ya utawala wa kisheria na uamuzi wa Allah, ambaye anamsha wishi yeyote amtakaye na kumwongoza yule anayemkusudia (Sura al- An„am 6:39; al-Ra„d 13:27; Ibrahim 14:4; al-Nahl 16:93; al-Fatir 35:8; al- Muddathir 74:31). Allah hafanyi agano na Waislamu. Anawachukulia kuwa watumwa wake. Yeye siye Baba, wala Mwokozi, wala Mfariji. Anamuangamiza yeyote asiyejiweka chini ya mapenzi yake (Sura al-Ra`d13:16; al-Zumar 39:4; al Hujurat49.14 na penginepo). Hata hivyo, atendaye (au atiiye), anatahiriwa kama alama ya uhusiano wake na Allah kama mtumwa. Tohara katika Uislamu ni mbadala wa ubatizo katika Ukristo.
1.11 -- Ubatizo – kiunganisho kuingia katika nguvu za Mungu
Mitume wa Yesu Kristo walibatizwa na Yohana Mbatizaji ndani ya mto wa Yordani. Hadharani walikiri dhambi zao na kuto kustahili kwao kuweza kusimama mbele za Mungu. Lakini Yesu aliwapa uhakika kwamba, watabatizwa kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, ili wasiendelee kuwa wadhaifu, wenye hofu na bila kufahamu, bali wapokee uongozi wa uwezo wa Mungu (Matendo ya Mitume 1:4-8; Yohana Mt. 1:33-34).
Katika lugha za kishemu neno linalotumika kwa ajili ya Mungu ni “El” likiwa na maana ya enzi na nguvu. Elohim ni aina ya wingi, na inaweza kutafsiriwa kama “Miungu wenye enzi.” Hata hivyo, neno “Allah” katika Uislamu ni aina ya umoja yaani moja kabisa isiogawanyika yenye maana: Yeye ndiye nguvu! Jina hilo kwa kiarabu katika maana yake ya kweli haliwezi kuonyesha Mungu wa Utatu. Linaweza tu kumaanisha Mmoja.
Yesu alishuhudia kwamba, mamlaka yote mbinguni na duniani alikabidhiwa Yeye. Yeye naye alifunua kwamba, Roho Mtakatifu ndiye nguvu ya Mungu. Mungu wetu ndiye nguvu ya namna tatu! Yeyote anayebatizwa ndani ya jina lake na kukubali mapendeleo haya, basi anadumu kwa kuunganishwa na njia ya nguvu ya Mungu. Atatoka katika hali yake ya kifo katika dhambi na kuingia katika uzima wa kiroho, naye atawaamsha wengine ambao bado wamo kifoni kwa ajili ya dhambi na udhalimu ili wahuishwe na Injili. Paulo alishuhudia wazi habari ya siri hii: “Siionei haya Injili, kwa sababu ni uweza wa Mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye ndani yake” (Warumi 1:16).
Petro aliwasihi Wayahudi walioshitukizwa: “Tubuni mkabatizwe kila mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu” (Matendo ya Mitume 2:38).
Yeyote aliyepokea nguvu ya Mungu kwa njia ya ubatizo na imani, basi haendelei kutumika katika nguvu zake mwenyewe, bali katika nguvu za Bwana, na atapokea uwezo na kuongezwa kila anapoomba ajaliwe nguvu na mengine anayohitaji. (Isaya 40:29- 31).
1.12 -- Kutii maagizo ya Kristo
Katika nchi za Kiarabu usemi huu “kutii neno la Mungu” inama anisha kujifunza hayo kimoyomoyo. Kwa uchache Waislamu wengi wanaifahamu Qur„ani kwa moyo, nzima au kwa sehemu. Mara nyingine wanatuuliza: kwa nini hatumpendi Mungu wetu, kwa sababu hatulitunzi neno lake! Kwao kujifunza ufunuo kwa kukariri kimoyomoyo ni uthibitisho wa upendo kwa Mungu. - Mkristo gani anajua injili moja au Hotuba ya Yesu Mlimani kwa kukariri kimoyomoyo? Kwa shida tu wachache wanakumbuka zaburi ya 23 au 103, aya za heri au labda Wakorintho wa kwanza sura ya 13. Wakristo wanatafakari mengi, bali wanakariri machache! Waislamu mara nyingi “wanajua”mengi, bali “ndaniyao hawatafakari”! Katika utamaduni wetu wa kufuata zaidi akili zetu tu, tungetubu na tusingesikiliza tu neno la Mungu, lakini tungelitunza zaidi na kufuata (Luka 11:28). Atakayejaza kumbukumbu zake kwa maneno mazito ya Biblia, atajaliwa nguvu nyingi kwa roho yake.
Kutunza tu peke yake, hata hivyo haitoshi. Yesu anatuambia wazi: “Mkinipenda, mtazishika amri zangu” (Yohana 14:15). Yepi hizo amri za Kristo? Sisi tumeongozwa kutafakari habari za neema, kujaliwa haki, kusamehewa, baraka na habari za Yesu mwenyewe; watu wachache tu wapo wanaochunguza sheria zake. Atakayesoma Injili zote nne kwa makini, ataweza kugundua kuna maagizo 500 halisi au yasiyo wazi sana, yaliyotajwa na Kristo. Baadhi yao yamejulikana sana na Wakristo, kama: “Wapendeni adui zenu! Waombeeni wanaowaudhi; watendeni mambo mema wale wanaowaumiza na kuwadhu lumu.” (Mathayo 5:44-47) - “Msamehe, kama Mungu alivyo wasamehe.” (Mathayo 6:12 na 14-15). – “Msihukumu, msije mkahukumiwa nanyi” (Mathayo 7:1-5).
Kuongoka kwa Kristo ni lazima kwa kila mtu. Hata hivyo, kubadilisha tabia ya maisha yetu pia ni agizo tukitaka kumfuata Kristo. Bila kujitakasa hakuna atakayemwona Bwana (Mathayo 5:8, 1.Wathessalonike 4:3; 1.Yohana 3:1-3).
Nani atathubutu kumfundisha mtu mwingine afuate amri za Yesu, akiwa mwenyewe bado hajayafuata? Wito wa Yesu kufundisha na kushika Neno lake katika maisha yetu ya kila siku ndiyo wito kwa walimu, wahubiri na wajumbe wa injili, watubu kwanza. Bwana hataki kusikia maneno matupu toka kwetu, bali anataka kuona kwamba tunatenda yale tunayoyatangaza. La sivyo, tuna futa maneno yetu kwa matendo yetu!
1.13 -- Tendeni yote niliyowaamuru!
Yesu alisema: “Mwafundishe kushika yote niliyowaamuru.” Neno hilo “yote” linaweza kutufanya tujisikie kama kuadhibiwa. Maana nani kati yetu anafahamu yote ambayo Yesu alituagiza tuya tende na kuyakumbuka kwa moyo? Nani anayaona amri zake zote mbele yake kila wakati? Nani anayafundisha yote kwa watoto wake mwenyewe, pia vikundi vya vijana na hata kwa kanisa nzima? Ni nani anayetimiza amri zote za Kristo kwa maneno, matendo na mawazoni kwa ukamilifu? Hakuna ataka yekuwa mwenye haki katika hayo yote. Sote tuna kosa kwa dai la neno hilo la Yesu. Hata yule mtakatifu mwema kabisa anaweza kutazama chini tu na kugugumia: “Bwana usinihukumu!” Zaidi ya hapo, tunapotafakari sana juu ya jumla ya maagizo yote ya Yesu, tutajisikia wanyonge sana. Yeye anasema: “Mwe watakatifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mtakatifu.” (Mathayo 5:48) “Hakuna atendaye mema, la, hata mmoja!” (Zaburi 14:3; Warumi 3:19-23; 7:3-8:4 na penginepo).
Sisi kama watumishi wa Kristo tunaendelea kuishi kila siku kwa sababu ya neema yake ya kutujalia haki, na tunahitaji kila siku kutakaswa kwa njia ya damu yake. Atakayesoma kwa makini 1.Yohana 1:7 hadi 2:6 na kwa kuomba, atagundua maelezo ya kufariji katika agizo hilo la Bwana kwetu.
1.14 -- Lengo ya amri (maagizo) ya Kristo ni nini?
Yesu anapenda kutuinua kwenye usawa na Baba yake. Ni lengo yake kwamba, ahadi ya msingi ya Mwumbaji wetu ipate kutimizwa ndani ya maisha yetu: “Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, kwa mfano wa Mungu alimwumba, mwanaume na mwanamke aliwaumba.” (Mwanzo 1:27) Yesu pekee aliweza kusema: “Aliyeniona mimi, amemwona Baba” (Yohana 14:9). Yeye anapenda kuwabadilisha wanafunzi wake ndani ya sura yake mwenyewe.
Katika Agano la Kale Mungu aliagiza: “Mwe watakatifu, kwa sababu mimi ni mtakatifu” (Mambo ya Walawi 11:44; 19:2) Yeye ndiye pekee kanuni ya kiroho kwa wote walioitwa naye.
Ndani ya Agano Jipya Yesu anaagiza: “Mpendane jinsi mimi nilivyowapenda ninyi!” (Yohana 13:14-15). Anafanya upendo wake kuwa kanuni kwa ajili ya upendo wetu kwa wengine. Yesu mwenyewe ndiye amri na mfano wetu. Paulo anaandika kwamba tumvaae Yesu ambaye ndiye uumbaji mpya. Basi tungefunikwa kabisa na Yeye. Tunao upendeleo wa kuwa “ndani ya Kristo” Tunaweza kuona kama mara 175 tamko hilo la kipekee ndani ya Agano Jipya. Paulo anatambua sana siri hii: “Mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita; tazama, yamekuwa mapya!” (2.Wakorintho 5:17).
1.15 -- Sheria ya Mhammad
Neno la Yesu: “Mwafundishe kuyashika yote niliyowaamuru ninyi” yangeweza kwa mabadilisho madogo kusomwa pia ndani ya Qur„ani! Hata hivyo kuna tofauti kubwa sana kati ya sheria ya Kristo na sheria ya Mhammad.Ni kweli kwamba, kuna aya kama 500 ndani ya Qur„ani zilichaguliwa na viongozi wa shule nne za sheria za Uislamu kama uti wa mgongo wa Shari„a. Lakini mle kuna aya zinayofanya nywele zetu kusimama wima, kwa mfano:
“Usimchukue adui yangu wala adui yako kuwa rafiki na usiwaonyeshe huruma!”" (Sura al-Mumtahana 60:1)
“Umwoe yeyote anayekupendeza kati ya wanawake: wawili, watatu au wanne kati yao. Lakini ukiogopa kwamba, huwezi kuwatendea haki, basi umwoe mmoja tu!” (Sura al-Nisa 4:3)
“Na kuhusu wale (wanawake) ambao unahofia kwamba watakuwa wakaidi: basi uwahubiri, uwaache peke yao kitandani mwao, na uwapige!” (Sura al-Nisa 4:34)
“(Allah alimwagiza Mhamadi:) Chukua kutoka kwa mali yao zawadi; kwa njia hii utawatakasa na kuwasafisha.” (Sura al Ma„ida 5:6; al-Tawba 9:103; al-A„la 8714 na penginepo)
“Katika habari ya mwizi, mwanaume au mwanamke: kata mikono yao miwili kwa hukumu.” (Sura al-Ma'ida 5:38).
Yeyote anayelinganisha sheria ya Kristo na sheria ya Mhammad atatambua kwamba, roho tofauti zinatawala ndani ya sheria hizo mbili. Katika sheria ya Mhammad hakuna upendo, hakuna upatanisho na Mungu, hakuna sadaka ya kujitoa kabisa kwa ajili ya wengine, wala hakuna utakatifu wa Mungu kama kanuni ya msingi kwa ajili ya wote.
Mwishowe, Mhammad mwenyewe ndiye kiini cha sheria yake. Maisha yake (Sunna) ilichukuliwa kuwa chemchemi au chanzo cha cha pili kwa ajili ya kuunganisha na kukamilisha sheria ya Uislamu. Kila Mwislamu angeishi jinsi Mhammad alivyoishi. Vinginevyo huyo sio Mwislamu safi. Mhammad alishiriki katika vita na ushindi mara 29, na pia alioa wanawake 12 au zaidi.
1.16 -- Kusudi la siri baina ya sheria ya Mhammad na ya Yesu
Kusudi ya sheria ya Uislamu, yaani Shari„a, ni usalama wa Umma ya Uislamu, ambayo ingefaa kuimarishwa kupitia serikali ya kidini, inayotawaliwa na Kiislamu. Uislamu sio dini inayotenganisha imani na siasa. Inaweza tu kuendeshwa vema, ikiwa imewekwa juu ya kanuni za Shari„a. Upande wa pili Shari„a inaweza tu kupata uimara ndani ya serikali ya kiislamu. Hivyo kusudi kuu ya Uislamu ni kufikia serikali ya kiislam. Namna yeyote nyingine ya Uislamu inahesabiwa ni kama hatua za kimkakati za awali za ki-mimba tu.
Kristo alitangaza kwamba: “Ufalme wangu si wa ulimwengu huu” ! (Yohana 18) Kanisa lake, kwa wale aliyewaita kutoka kwenye mataifa mbalimbali, ndiyo wanaounda ufalme wake wa kiroho katika mazingira yao kadhaa. Ushirikiano wa wanafunzi wake ndiyo mwanzo wa ufalme wake wa milele (Yohana 13:34- 35). Wanahimizwa kuwa kama “chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu.” Sheria ya Yesu haina lengo la kusimamisha serikali ya kidini ya kikristo, bali kuwabadilisha wafuasi wake watii maagizo yake na kuwashawishi jamii ambazo wanaishi nazo pamoja na serekali.
1.17 -- Mimi nipo pamoja nanyi!
Kama mjumbe wa Yesu Kristo anajinyenyekeza na kutambua kutokuweza kwake na udhaifu wake, na anapokiri hali yake hiyo, ndipo Yesu anamwambia: “Fungua macho yako! Tazama! Mimi nipo hapa! Naishi! Mimi naishi kwa uhakika! Sitakuacha peke yako! Mimi nakupenda! Nami nakusaidia! Nitakuimarisha na kukushika daima!”
Kuna usemi juu ya Yesu kwamba, wakati fulani alimwonyesha mfuasi wake mmoja ndani ya ndoto njia mbili za nyayo ndani ya mchanga mnyevu akimweleza: “Tazama, nimekusindikiza kwa uaminifu tangu muda mrefu.” Wakati njia ile ya pili ilipopotea mahali pa miamba ya hatari, yule mwenye ndoto akauliza kwa kushutumu: “Kwa nini umeniacha peke yangu mahali pagumu pa kukuhitaji hasa? Ndipo Bwana akamjibu: “Hapo nimekubeba hadi nja ilipokuwa safi tena.” Upendo wa Kristo ni mkubwa kuliko mawazo yetu. Alimthibitishia mjumbe wake kwamba: “Hakuna awezaye kuwapokonya mkononi mwangu!” (Yohana 10:28). Kuwepo kwa Yesu Mwenye Uwezo wote na uwenyezi wake huo, ungetutia moyo tuwe na imani imara kabisa na kuendelea kumtumikia kwa furaha mbele ya uso wake.
1.18 -- Hadi mwisho wa ulimwengu wote
Siku hizi maelfu ya wamisionari wageni na Wakristo wenyeji wengi sana zaidi katika nchi mbali mbali nyingi wanamtumikia Bwana Yesu Kristo kwa uaminifu, hata katika maeneo yanayoongozwa na kutawaliwa na roho zilizo kinyume na ukristo. Makanisa yamechomwa moto na Wakristo wenye bidii wamesingiziwa, wametishwa na kudhulumiwa. Wengine wame toroka kwao au wakateswa.Wengi wanaishi mafichoni. Hofu mara nyingi inawafanya wafadhaike.
Hata hivyo Yesu anatuhakikishia kwamba: “Linalowapiga wao, limenipiga mimi kwanza!” Maumivu katika kiungo cha mwili kwanza inaingia ubongoni, hata kabla ya mwili kuisikia. Kristo akiwa kichwa cha kanisa ndiye wa kwanza anayesikia mateso ya watumishi wake, hata kabla ya wao wenyewe kutambua. (Matendo ya Mitume 9:4-5). Hakuna kati yetu aliye peke yake. Mwana Kondoo wa Mungu anatembea pamoja nasi kwenye njia ya mateso hadi mwisho. Siku hizi kuna mateso mengi zaidi, lakini pia kuna matukuzo mengi kwa ajili ya Yesu kuliko tunavyotambua.
1.19 -- Hadi mwisho wa dahari!
Wakati wa ubatizo wako Yesu alikupatia ahadi ya uhakika kabisa atakuwa pamoja nawe kila dakika ya maisha yako, ikiwa wewe unaendelea pamoja naye na kumtumikia. Hata katika hatari kubwa kabisa na saa ya kufa Yeye atakuwa karibu nawe. Yeye anakuhakikishia: “Mimi ndimi huo ufufuo na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi, na kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je, unayasadiki hayo?” (Yohana 11:25-26). Yesu anataka kukubeba hadi utaka pozeeka na kukaa nawe hata saa ya kuondoka ulimwenguni huu (Zaburi 23:4-6).
1.20 -- Je, Allah yu pamoja na Waislamu wake?
Ndani ya Qur„ani imeandikwa kwamba, wakati ilipompasa Mhammad kutoroka kutoka Maka kwenda Medina, njiani alijikinga ndani ya pango na kumwambia Abu Bakr: “Kweli, Allah yu pamoja nasi!” Waislamu walioonewa walijisikia bora sana zaidi baada ya hapo (Sura ai-Tawba 9:40).
Bahati mbaya, Allah huyu, aliyekuwa amemfariji Mhammad, huyo siye Mungu wa kweli, kwa sababu Allah asema mara 17 ndani ya Qur„ani kwamba, yeye hakuwa na mwana, na kwamba Kristo hakufa msalabani (Sura al-Nisa 4:157). Baba wa Yesu Kristo hayuko pamoja na Waislamu. Wanakataa kifo cha sadaka ya kafara cha Yesu na wanadai kwamba, roho fulani asiyejulikana, aitwaye Jibril (Gabrieli) angeweza kuwa Roho Mtakatifu. Roho inayowaendesha Waislamu inawatikisa na kuwaendesha katika chuki kinyume cha kabisa na Ukristo. - Sisi tunaamini kwamba, mbali na Baba, Mwana na Roho Mtakatifu hakuna Mungu mwingine.
1.21 -- Nene “wote” lipo mara nne katika Agizo la utume mkuu
Aishivyo Yesu anawahakikishia wanafunzi wake kwamba, mamlaka YOTE mbinguni na duniani amepewa yeye Kristo. Kwa sababu hiyo waende na kuwafanya wanafunzi wa mataifa YOTE wakiwabatiza katika jina la Baba, la Mwana na la Roho Mtakatifu. Ndipo wawafundishe hao waumini waliobatizwa washike maagizo yake YOTE. Ndipo alipowaahidi watumishi wake kwamba, atakuwa pamoja nao siku ZOTE hata ukamilifu wa dahari (Mathayo 28:18-20).
Basi, Yesu anakutia moyo wewe, upate kumtegemea na kumtumainia pia kwa sababu ya neno lake la YOTE mara nne nawe utimize maagizo yake; naye hatamwacha yeyote kati ya watumishi wake peke yake. Ndiposa mwishoni na wewe pia utamwona.
1.22 -- MASWALI
Mpendwa Msomaji !
Kama umejifunza kitabu hiki kwa bidii, bila shaka utaweza kwa urahisi kujibu maswali yafuatayo hapi chini. Kila mmoja ataka yejibu 90% ya maswali yote ndani ya hivi vitabu 8 vya mfululizo huu kwa ufasaha, atapokea cheti kutoka kwenye kituo chetu,
Mafunzo endelevu
katika njia ya kusaidia kuendesha mazungumzo na Waislamu kuhusu Yesu Kristo.
Hii itakutia moyo kwa ajili ya kuendelea katika kumtumikia Kristo
- Bwana Yesu anatoa nini kwa ajili ya ulimwengu baada ya kufa na kufufuka kwake?
- Ni nani anayestahili kutumika kama mjumbe wa Yesu Kristo?
- Kwa nini Yesu aliwapa changamoto hata wale wenye mashaka kati ya wafuasi wake waitike kwa Agizo lake Kuu?
- Ina maana gani kwamba, Yesu alipokea mamlaka yote mbinguni na duniani?
- Kwa nini Baba wa mbinguni hakuhofia kwamba, Mwana wake angekuwa mkaidi dhidi yake baada ya kumkabidhi mamlaka yote na enzi?
- Kwa nini Yesu anawaagiza wafuasi wake “waende” wala si “wakae na kutulia”?
- Jinsi gani utaweza kumwona mtu anayengojea ushuhuda wako, na jinsi gani inakupasa kuzungumza naye?
- Namna gani utaweza kukusanya wanafunzi wakuzunguke wewe? Na unaweza kuwatolea nini wasikikilizaji wako?
- Kwa nini Agizo la utume mkuu unatuelekeza hata kwa watoto wa Ishmaeli na watoto wa Yakobo? Nchi gani au dini gani zimetengwa na huu mpango mtukufu (wa Agizo Kuu)?
- Sehemu gani ya moja kwa mia (%) ya wakaaji wote wa ulim wenguni wanajiita Wakristo siku hizi? Na hali halisi hiyo ina maana gani kwako wewe?
- Nini ni maana ya ubatizo katika jina la Baba na Mwana na Roho Mtakatifu?
- Jinsi gani ule Umoja wa Utatu Mtakatifu unajitokeza ndani ya AGIZO LA UTUME MKUU?
- Namna gani utaweza kupokea nguvu na uongozi katika utumishi wako kwa ajili ya Kristo?
- Kwa nini ubatizo na kuzaliwa mara ya pili sio mwisho bali mwanzo wa maisha ya kikristo?
- Mambo gani ni tofauti kati ya kuwahubiri watu wasio Wakristo na kuwafundisha waumini? Na jambo hilo lina maana gani katika mazungumzo yako na Waislamu?
- Mambo gani tungefundisha kwa waumini waliokwisha kubatizwa?
- Maagizo mangapi ya Kristo unaweza kugundua ndani ya Injili zote nne? Na katika hayo ni yapi unayoona ni muhimu zaidi kwa ajili ya Mwislamu?
- Ipi ni tofauti kati ya hali ya kuhesabiwa haki kwa imani tu na ulazima usiokwepeka wa kutenda matendo mema kwa sababu ya utii wa imani iliyo zawadi ya neema?
- Nini ni kanuni ya pekee kuhusu sheria (maagizo) ndani ya Agano Jipya?
- Kwa nini sheria ya utatu ndani ya Wito Kuu unavunja kiburi ya kila mwalimu,mtumishi au mtakatifu, kama anajiona mwaminifu mbele zake mwenyewe?
- Jinsi gani Yesu aliweza kuahidi: “Tazameni, mimi nipo pamoja nanyi”?
- Kwa nini Yesu anaahidi kuwa pamoja nawe popote na siku zote, ukitumika katika jina lake?
- Kwa nini Waislamu wanaweza kuamini kwamba, Kristo (`Isa) yu hai pamoja na Allah?
- Kwa nini haiwezekani kwa Mwislamu kuwaza kwamba miungu wawili wanaweza kuishi pamoja kwa amani milele? Kwa nini hilo si shida kuamini kwa Mkristo?
- Andika Agizo Kuu la Waislamu kinaganaga (ukinukulu Sura na mstari ndani ya Kurani), ndipo ulinganishe na Agizo Kuu la kikristo.
- Waislamu walielekea wapi na ndani ya nchi gani katika mawimbi yao kueneza dini yao, na sehemu gani ya moja kwa mia (%) ya watu wote duniani ni Waislamu siku hizi? Waislamu wangapi wanaishi katika nchi yako?
- Ina maana gani kwa Mwislamu kuwa mvumilivu kwa washiriki wa dini zingine na uvumilivu huu unaweza kwenda kwa kiwango gani? Lini itampasa aanze kutokuvumilia?
- Kwa nini Mhammad alikataa Umoja wa Mungu katika Utatu Utakatifu?
- Qur„ani inasema nini kuhusu ubatizo katika Ukristo?
- Zipi ni baadhi ya tofauti muhimu kati ya Amri za Mhammad (Shari„a) na za Amri za Kristo ndani ya Injili?
- Ipi ni shabaha ya Amri za kiislamu, na ipi ni shabaha ya Amri za Kristo?
- Ina maana gani kwa Mwislamu kwamba, Mhammad ndiye kanuni kwa Amri za kiislamu?
- Kwa nini Mhammad hakuweza kuwaahidi wafuasi wake: “Tazameni, mimi nipo pamoja nanyi kila siku hadi mwisho wa nyakati”?
- Ile maana ya neno la “WOTE” (wote, yote, zote) ya mara nne ndani ya Agizo ya utume Mkuu ni nini?
Kila mshiriki katika maswali haya hii anaruhusiwa kutumia kitabu chochote apatacho, pia na kumwuliza mtu yeyote mwaminifu anayemfahamu, anapojibu maswali hayo. Sisi tunangojea majibu yako yakiwa yameandikwa pamoja na jina na anwani yako kwenye karatasi au katika e- mail kutoka kwako. Tunakuombea kwa Yesu, aliye Bwana aliye Hai, aweze kukuita na kukutuma, akuongoze, akutie nguvu, akulinde na kuwa karibu nawe kila siku ya maisha yako mbeleni!
Wako katika utumishi wa Bwana,
Abd al-Masih and his brothers
Tuma majibu yako kwa anwani hii:
GRACE AND TRUTH
P.O.Box 1806
70708 Fellbach
GERMANY
or by e-mail to:
info@grace-and-truth.net