Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 077 (Challenges to the validity of the Bible as Muslims believe it has been abrogated by the Qur’an)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO

13.2. Changamoto juu ya Uhalali wa Biblia maana Waislamu wanaamini imekwisha kufutwa na kubadilishwa na Qur’an


Sehemu ya pili ya changamoto kwa Ukristo inakuja kupitia dhana ya Uislamu ya kutenguliwa. Hii ni imani inayosema Qur’an inafuta kabisa vitabu vyote vya KiMungu vilivyokuja kabla yake. Ingawa haijaelezwa wazi wazi kwenye Qur’an au Hadith, Inapendekezwa katika aya ya Qur’an na hadith. Qur’an inasema:

“Na anayetafuta dini isiyo kuwa Uislamu haitakubaliwa kwake. Naye Akhera atakuwa katika wenye Kukhasiri” ( Qur’an 3:85)

Kwa kuongezea Muhammad alisema:

“Kwa Yule ambaye mkono wake ni maisha ya Muhammad, yoyote miongoni mwa jamii ya Wayahudi na Wakristo wakisikia juu yangu, na imani yake haikubaliani na na ambayo niliyotumwa nayo na akafa katika hali hiyo (ya kutoamini), atakuwa bali katika miongoni mwa watu wa motoni.” (Sahih Muslim).

Waislamu wanaamini kwamba Uislamu pekee unakubalika kwa Allah, ambayo inamaanisha kwa Waislamu kwamba dini zingine zote zimetenguliwa na Qur’an.

Kutathimini madai hayo na tufahamu kwanza inamaanisha nini neno kutenguliwa. Kutangua kitu ni kufuta, kukomesha, kubatilisha, kuondoa na kadhalika. Katika muktadha huu, kutangua inaweza kufanyika kwenye sheria na kanuni lakini haiwezi kufanyika kwenye matukio ya kihistoria, ndio kumaanisha Qur’an haiwezi kubadilisha matukio ya Kihistoria yaliyotokea kabla yake. Hata hivyo, tunaposoma Qur’an tunakutana na kinyume kabisa na haya- Qur’an ilibadilisha habari inayohusika na Kutoka! Qur’an inasema Msamaria aliwapotosha Waisrael na kuwafanya waabudu ndama, ingawa Samaria hata haikuwepo wakati wa Kutoka.

Sio kwamba tu Qur’an inabadilisha historia, pia inachanganya matukio kadhaa za ki-historia pamoja. Kwa mfano, katika aya moja inachanganya nyakati tatu za kihistoria pamoja. Inamnukuu farao wakati wa Musa akisema:

“Ewe Haman! Nijengee mnara ili nipate kuzifikia njia” (Qur’an 40:36)

Hata hivyo Farao aliishi zaidi ya miaka elfu moja kabla ya Haman (Waziri wa Ahusuero anayetajwa kwenye kitabu cha Esta), na zaidi ya miaka elfu kabla ya ujenzi wa mnara wa babeli katika jaribio la kufika mbinguni ( Mnara wa Babeli umeelezwa katika Mwanzo 11).

Waislamu wa leo wanajaribu kukwepa hili kwa kueleza kwamba “Haman” ni maneno mawili “Ha Man” kutokana na “Ha- Aamon” kuhani mkuu wa Amon.Bahati mbaya bila shaka hakuna sio matendo wala nini kinachotatua tatizo hili. Haiwezi kufanya kazi kwa sababu Wamisri wasingeweza kutumia silabi ya erufi ya Kiebrania “Ha”. Na hata kama hii ingekuwa ya kweli (Sio ya kweli), Bado tunatakiwa kueleza kwa nini amewekwa katika wakati mmoja na Mnara wa Babeli.

Mfano mwingine wa makosa katika Uislamu ni pale Qur’an inaposema kwamba mmojawapo katika watoto wa Nuhu alizama katika gharika (Qur’an 11:42). Tunajua kulingana na Biblia kwamba familia yake nzima ilikuwa hai baada ya gharika.

Madai mengine ya Qur’an yanayopingana na matukio ya Kihistoria katika Biblia yanajumuisha Ayubu Kuelezwa kama uzao wa Isaka (Qur’an 6:84), Ishamael kuwa nabii na Mtume (Qur’an19:54), na kukana kusulubiwa (Qur’an 4:157).Wakati inakubalika kwamba amri zinaweza kutenguliwa, lakini haiwezekani matukio halisi ya ki-historia yaliyotokea kutenguliwa. Zaidi matukio mengi katika Qur’an hayako wazi na yanaweza kufahamika kupitia Biblia tu.

Dhana ya kutenguliwa haipo tu kwa vitabu vya mwanzo, lakini kwa sehemu za mwanzo za Qur’an ambayo zinapingana na sehemu zilizoandikwa baadaye. Hiyo ni kusema inaweza kuwa dhana ya kukubalika katika mafundisho ya Kiislamu maana bila hiyo kungekuwa na kupingana kwingi sana katika Qur’an ili iweze kukubalika na kutegemewa. Ingawa hatuwezi kutaja yote hapa, Miongoni mwa vitu vilivyotenguliwa ni vitu ambavyo kimsingi Muhammad aliviamiani kuwa sehemu ya Qur’an na kwamba vimefunuliwa kwake na Allah lakini baadaye yakadaiwa kutoka kwa shetani:

“Na hatukumtuma kabla yako Mtume wala nabii ila anaposoma, shetani hutumbukiza (Uongo) katika masomo yake.Lakini Allah huyaondoa anayoyatia shetani. Kisha Allah huzithibitisha aya zake.Na Allah ni Mjuzi na mwenye hekima.” (Qur’an 22:52)

Aya hizi basi zinahitajika kutenguliwa. Hata hivyo tatizo hili halina cha kufanya na Biblia kivyovyote vile. Miongoni mwa sintofahamu nyingi za Waislamu juu ya Biblia wanafikiri ipo au inafanya kazi kama Qur’an; Na hii si kweli kabisa. Biblia iliandikwa kufundisha waamini ambao waliamini kutokana na waliyoyaona na kuyasikia, Kama ni wakati wa Musa na Manabii katika Agano la Kale au katika nyakati za Mitume wa Agano Jipya. Haikuandikwa kutoa changamoto kwa wasioamini au kuwafanya watu waamini. Katika Biblia unafanywa mwamini na Roho Mtakatifu kukushawishi na Baba kukupa hakika ya Msamaha.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:43 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)