Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 078 (Objections to the trinity)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO

13.3. Mapingamizi juu ya Utatu


Pingamini la tatu ambalo tutaitazama ni pingamizi juu ya Utatu. Ingawa Waislamu wanapinga dhana ya Utatu wa Kikristo, Qur’an na Hadith zinapinga kitu tofauti kabisa. Qur’an inawashutumu Wakristo kuabudu miungu wawili Yesu na Mariamu mbali na Allah (Qur’an 5:73, 4:171). Hata Waislamu wa sasa, wanapoongelea Utatu wanadai kwamba Ukristo unafundisha kwamba Mungu ni nafsi tatu katika nafsi moja. Hivi ndivyo watetezi wa Kiislamu wanavyoiweka:

“Kulingana katekisimo ya Kanisa La Wakristo, Baba ni nafsi, Mwana ni nafsi, Roho Mtakatifu ni nafsi; Lakini sio watatu bali mmoja” (Dr. Zakir Naik, Dhana ya Utatu!!- hutuba iliyotolewa 2012)

Hata hivyo kila Mkristo anajua kwamba hakuna Katekisimo yoyote ya kanisa inayosema hivyo, badala yake Wakristo wanasema Mungu ni nafsi tatu katika umoja wa “nguvu” au “Asili”. Wakristo hawajawahi kusema kwamba nafsi tatu ni nafsi moja badala yake Mmoja mwenye nafsi tatu.

Kama wanadamu hatuna haki, mamlaka, wala uwezo wa kumwmabia Mungu yeye ni nani. Hivyo tunatakiwa tu kuchukua neno la Mungu kama mamlaka yetu ya kutuambia Mungu ni nani. Katika Biblia kutoka mwanzo kabisa Mungu anadhihirishwa kama Mungu mmoja:

“Sikiza, Ee Israel; BWANA, Mungu wetu, BWANA ndiye mmoja” (Kumbukumbu 6:4; Marko 12:29).

Fundisho hili ni la msingi sana Katika Ukristo na Biblia inasisitiza juu yake. Mtume Paulo anasema:

“Na kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani na wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia imani iyo hiyo” (Warumi 3:30),

na

“Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Yesu Kristo” (1 Timotheo 2:5).

Kwa wakati huo huo Biblia haileti Moja kama moja iliyo moja tu bali moja yenye umoja. Aya katika Kumbukumbu inatumia neno Echad “אֶחָֽד”. Neno hili katika Biblia inatumika mara kwa mara kuonyesha Muunganiko kama ilivyo atika Mwanzo 2:24 “Watakuwa mwili mmoja” Mwanzo 11:6 “Kundi moja” Kutoka 36:13“Maskani moja”, Kutoka 23:29 “Mwaka mmoja” na kadhalika. Kuna neno lingine la Kiebrania inayomaanisha moja: yachid “יָחִיד”. Hii neno kabisa inamaanisha nambari moja kama ilivyo katika Waamuzi 11:34 “Mwanaye na wa pekee” na Mithali 4:3 “wa pekee”. Hili neno halijawahi kutumika juu ya Mungu popote pale kwenye Biblia.

Je Biblia inasema nini juu ya nafsi tatu za Mungu?

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 01:47 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)