Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 083 (The Claim of prophecies about Mohammed in the Bible)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO

13.5. Madai ya Unabii juu ya Muhammad katika Biblia


Mada ya mwisho na ya tano tutaangalia mazingatio ya tafsiri za Waislamu juu ya baadhi ya sehemu za Biblia ambayo wamechukulia kumaanisha kitu kingine tofauti na ufahamu wa Mkristo.Sehemu zizodaiwa kumuongelea Muhammad, kulingana na aya ya Qur’an ambayo Yesu aliwaambiwa Waisrael:

“Enyi wana wa Israel! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, Ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Torati, na mwenye kubashiria kuja kwa Mtume baada yangu; jina lake Ahmad.” (Qur’an 61:6)

Jina Ahmad ina mzizi wa maneno katika kiarabu kama Muhammad, na ndio imechukuliwa kwamba inamuongelea Muhammad. Kama matokeo ya haya, Waislamu kwa ujumla wao wanaamini kwamba lazima kuwe na unabii juu ya Muhammad ndani ya Biblia. Wengine wanafikiri Wayahudi na Wakristo wameyaondoa wakati wengine wanafikiri bado zipo na unatakiwa tu kufungua na kunyonya maandiko. Kuna mamia ya vitabu kuhusu hili, yanayoelezea aya za Biblia zinazodhaniwa kumuongelea Muhammad.

Miongoni mwa unabii unaosemekana kumhusu Muhammad ni za kipuuzi. Chukulia mfano wa maneno ya Yesu katika Yohana 14:30:

“Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, Kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu.”

Baadhi ya Wanazuoni wa Kiislamu wanaona hii kama unabii juu ya Muhamamad. Bila shaka waislamu hawaoni upuuzi wa jambo hili maana hawajui kwamba cheo hicho kinatumika kumaanisha shetani kwenye Biblia!

Nyingi katika hizi zinazodaiwa kuwa unabii haziwalengi Wakristo waamini ambao wanaijua Biblia. Zinawalenga Waislamu au wakristo wa jina ambao hawajui lolote kuhusu Biblia. Zote katika hizi zinazoitwa unabii zinatumia mtindo ule ule wa Kusoma vibaya maandiko ya Biblia (ama kwa makusudi au kwa kutokujua), au kwa kuchagua na kuchukua mistari au hata maneno na kuzipindisha ili kufanya ziwe na maana wanayotaka. Mfano wa hili ni Kumbukumbu 18:18 wakati Mungu alipomwambia Musa:

“Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, na atawambia yote nitakayomwamuru.”

Waislamu wanasema kwamba “miongoni mwa ndugu zao” inamaanisha Mwarabu kwa sababu Waarabu- ni uzao wa Ishmael kaka yake Isaka- ni ndugu.Hivyo basi nabii wa namna hiyo hawezi kuwa Muisrael bali lazima awe Muarabu. Kuna shida moja ya namna hii ya kutoa hoja:Israel inaitwa hivyo kwa sababu wao ni uzao wa mtu mmoja Israel (Yakobo), sio kwa sababu ya Isaka, na Ishmael alikuwa kaka wa kambo wa baba mwanzilishi wao hivyo basi sio babu wa moja kwa moja wa waisrael. Kama miongoni mwa ndugu zao haikumaanisha Muisrael, basi ingeleta maana kwenda kwa Waedom, uzao wa Esau, Kaka pacha wa Yakobo, ambapo ni mahusihano ya karibu kuliko Waarabu.

Lakini pia tunawauliza Waislamu kwa nini wanaamini zinazodaiwa kuwa unabii wakati wanaamini Biblia iliharibiwa? Kwani nini tuamini unabii wa kitabu kilichoharibiwa? Na kama wanaziamini kwa nini sasa wakatae zingine zilizobaki? Katika hatua hii waislamu wanadai kwamba sio Biblia yote iliyoharibiwa bali sehemu kadhaa tu. Ilibadilishwa sehemu tu zile zinazopingana na Uislamu. Haya ni madai ya kipuuzi ambayo hayaungwi mkono na ushahidi wowote ule. Je isingekuwa rahisi Wakristo kufanya kama Wayahudi walivyofanya? Kuacha unabii kwenye maandiko, kisha kusema hazimaanishi vile tunavyodhani inamaanisha? Hata hivyo hivyo, Wayahudi hawajaiondoa Isaya 53 kutoka kwenye Biblia yao; badala yake wanaileza tofauti au wanajaribu kuipa tafsiri nyingine. Zaidi sana; kipi kiwasukume Wayahudi na Wakristo kukana unabii wa Muhammad? Kwa akili ya kawaida lazima kuwe na sababu. Je tunapaswa kuamini kwamba kuna watu waliobadilisha unabii wa mtu ambaye angekuja miaka mamia na maelfu ijayo- kwa kurejea Agano la Kale na kufanya wakalaaniwa na kupoteza uzima wa milele- na uzao wao kupoteza maisha, au kuwa watumwa na ama kuwa raia wa daraja la pili? Hivyo wapoteze maisha haya na maisha ya ulimwengu ujao kwa sababu zipi? Wapoteze uzima wa milele, na wapoteze upendeleo mkuu kama wangekubali na kuwa Waislamu- je hiyo inaingia akilini? Hatupaswi kuchoka kuwasaidia Waislamu kufikiri kwa umakini sana madai yao, na kinachofundishwa na Uislamu kuhusu maisha haya na maisha ya ulimwengu ujao, Tukitumaini kwamba Mungu atawajalia toba katika kumjua Kristo.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 02:17 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)