Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 082 (Objections about Christ's crucifixion and resurrection)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO

13.4. Mapingamizi juu ya Kusulubiwa na kufufuka kwa Kristo


Baada ya kujadili mapingamizi matatu ya kawaida, ngoja sasa tuangazie pingamizi nyingine mbayo inashikiliwa na Imani ya Kiislamu. Inayosema kwamba kulikuwa kweli na kusulubiwa lakini hakuwa Yesu msalabani lakini badala yake mtu mwingine aliyefanana naye tu.

Kwa kweli kuna aya moja tu ndani ya Qur’an juu ya kusulubiwa, na aya hii ina utata katika lugha ya Kiarabu. Tafsiri ya moja moja ya aya hii inasema:

“Na kwa kusema kwao: Sisi tumemuuwa Masih Isa bin Maryamu, Mtume wa Mwenyezi Mungu- nao hawakumuua wala hawakumsulubu, bali walifafananishiwa tu. Na kwa hakika walio khitalafiana katika haya wamo katika shaka nayo. Wao hawana ujuzi nayo wowote, ila ni kufuata dhana tu. Wala hwakumuua kwa yakini.” (Qur’an 4:157)

Maneno hapa yaliyotafsiriwa kama “Walifananishiwa” (shubbiha lahum) yametafsiriwa tofauti kama:

  1. Sahih International: “Mwingine alifanywa afanane naye kwao”
  2. Pickthall: “Lakini ikaonekana hivyo kwao”
  3. Yusuf Ali: “Hivyo ilifanywa ionekane hivyo kwao”
  4. Shakir: “Lakini ikaonekana kwao hivyo (kama Isa)”
  5. Muhammad Sarwar: “Wao, kwa kweli, walimuua mtu mwingine Kimakosa”
  6. Mohsin Khan: “Lakini mfano wa Isa (Yesu) uliwekwa juu ya mtu mwingine (Na wakamuua huyo mtu)"
  7. Arberry: “mfano pekee wa hilo ilionyeshwa kwao”
  8. Kamal Omar: “Na badala yake imebaki tukio la shaka kwao”
  9. Mohammed Ahmed & Samira: “Lakini ilifanana/ Isiyoeleweka/ walikuwa katika shaka”
  10. Wahiduddin Khan: “Lakini ilionekana tu kwao [kana kwamba imekuwa hivyo]"
  11. Qaribullah & Darwish: “Lakini kwao, yeye (aliyesulubiwa) alipewa muonekano (wa nabii Yesu)”
  12. Maududi: “Lakini sula hili ilifanywa kwao ni yenye mashaka”
  13. Asad: “lakini ilionekana kwao [ kama imekuwa hivyo] hivyo”
  14. Khatab: “Ilifanywa ionekane hivyo”
  15. Malik: “Lakini walifikiri wamefanya kwa sababu jambo lenyewe lilifanywa isiyoeleweka kwao”
  16. Laela Bakhtiar: “Badala yake mfano wake kwa mwingine ulionyeshwa kwao”
  17. T.B. Irving: “hata hivyo ilionekana kwao hivyo”
  18. Unman: “Lakini walidanganywa kwa muonekano”
  19. Bijan Moeinian: “Matamanio ya fikra zao zimetengeneza mkanganyiko sana na kukosa kwa ushahidi wa kihistoria kwa wanayoyasema”
  20. Amatul Rahaman Omar: “alifanywa kwao kufanana ( na aliyesulubiwa)”

Hivyo unaweza kuona kwamba hakuna makubaliano ya wazi juu ya maana halisi. Haya maneno yametafsiriwa kwa namna tofauti zaidi ya ishirini kwa namna yoyote ile kutoka “Ilionekana kwao” hadi Matamanio ya fikra zao zimetengeneza mkanganyiko sana na kukosa kwa ushahidi wa kihistoria kwa wanayoyasema” Mkanganyiko huo pia unaonekana kwenye mafafanuzi ya Qur’an; wengine wanatambua kwamba mtu mwingine alichukua nafasi ya Kristo, Wengine wanasema huyo mtu alikuwa Yuda Iskariote, na bado wengine wanasema alikuwa ni Yesu lakini hakufa.

Mfafanuzi wa Qur’an al-Razi katika mafafanuzi yake kwa aya hii aliuliza maswali mazuri sana kuhusu mtu mwingine kuchukua muonekano wa Yesu.

  1. Tukiruhusu dhana hii ya kubadilika kwa muonekano, itatuongoza kwenye mazingaombwe. Hivyo hivyo, kama nikimuona mtoto wangu mara moja, wakati mwingine nikimumona sitakuwa na uhakika kama ni mtoto wangu- anaweza kuwa mtu mwingine anayefanana naye. Hiyo itaangamiza kuaminiana katika fahamu zetu. Zaidi Masahaba wa Mtume waliomuona akiwafundisha- Labda huyo hakuwa Muhammad bali ni mtu mwingine ambaye alionekana kama yeye.
  2. Qur’an inasema kwamba Yesu alisaidiwa na roho takatifu “Jibril”, iliwezekanaje asimuokoe bila uhitaji wa kumuua mtu mwingine?
  3. Yesu alikuwa na uwezo wa kufufua wafu, kwa nini asingejiokoa mwenyewe?
  4. Kama mtu mwingine ndiye aliyekufa mahali pa Yesu na alipaishwa hadi mbinguni bila kufa, kwa kufanya hivyo kila mtu kaamini kwamba alikuwa msalabani na akafufuka kutoka kwa wafu:Hii inamaanisha Allah aliwadanganya na kuwafanya waamini katika uongo.
  5. Wakristo kila mahali, pamoja na upendo wao na heshima yao kwa Kristo, wanakubali kwamba alikuwa msalabani. Hii sio kitu ambacho kingetengenezwa kudanganya, hivyo tuna kila sababu kuwaamini kuliko mashahidi wengine kwa manabii.
  6. Imethibitishwa kwa hakika kwamba yule mtu aliyekuwa juu ya msalaba alikuwa juu ya msalaba kwa masaa mengi; kama asingekuwa Yesu, basi angesema hivyo. Hii haikutokea.

Razi anajaribu kuelezea maswali yake mwenyewe na majibu yake ya kijinga, kama kusema “Kama Jibril angemuokoa Yesu, hiyo ingefanya muujiza wa Yesu kuwa mkubwa ambapo ingefikia kiwango cha kuwalazimisha watu kuamini, ambayo sio halali”. Mwishoni anamalizia kwa kukubali kwamba amekataa hitimisho la kiakili kwa maswali yake yote: Sababu take ni Qur’an inasema vinginevyo!

Kusulubiwa kwa Yesu ni tukio la kweli la Kihistoria ambayo hata wasiomuamini Mungu leo hii hawawezi kukataa. Bart Ehrman (ambaye hajulikani kabisa kwamba kama amekabidhi maisha yake Kwa Kristo) kwa mfano anasema “Kusulubiwa kwa Kristo kwa amri ya Pontio Pilato ndio tukio lililo wazi zaidi kuhusu yeye (Utangulizi mfupi wa Agano Jipya). Ni ukweli usiopingika, Je tunapaswa kupinga au kuishakia kwa sababu mtu mmoja alikuja baadaye miaka mia sita na kusema maneno mawili ambayo hata wafuasi wake wenyewe hawayafahamu lakini wanadhani kwamba yanaweza kumaanisha kwamba hakuwa Yesu juu ya msalaba bali mtu mwingine aliyefanana na yeye.Kweli? Je Waislamu wangeweza kuchukuliana na dhana ya kipuuzi namna hiyo kama ingehusishwa na Muhammad? Qur’an na historia ya Kiislamu inasema Muhammad alikuwa amejificha ndani ya pango pamoja Abubakar alipokuwa akitoroka kutoka Maka kwenda Madina (Qur’an 9:40). Je vipi tukisema walipotoka pangoni hakuwa Muhammad mwenyewe lakini mtu mwingine aliyeonekana machoni kwa Abubakar kama Muhammad. Hata hivyo aya za Qur’an zilizoandikwa na huyu mtu baada kutoka pangoni ni tofauti sana na zile zilizoandikwa kwa mkono huko Maka. Tunaona badiliko ya tabia kwa sababu Muhammad alikuwa katili zaidi baada ya tukio hili la pango. Alibadilisha malengo yake; kwani akawa mtu wa vita katika kipindi cha mwaka mmoja alianza kuvamia makabila mengine wakati hakuwahi kumshambulia yoyote kabla. Je Waislamu wanaweza kudhani dhana kama hiyo inaweza kuchukuliwa kwa umakini? Bila shaka hapana! Hivyo ndivyo Wakristo wanavyohisi tunaposikia “Ilionekana kwao kama” mwisho wa aya inasema “ wale wanaotofautiana wako katika shaka kwayo” hawana ufahamu nalo, lakini wanafuata dhana tu”. Lakini kama tulivyoona ni Waislamu ndio wenye shaka na wanaotofautiana, Wakristo katika historia yote wamekuwa na makubaliano na ukweli huu wakati wote:

“Kwamba Kristo alikufa kwa ajili ya dhambi zetu, kama yanenavyo maandiko matakatifu;na ya kuwa alizikwa; na alifufuka siku ya tatu, kama yanenavyo maandiko, na ya kuwa alimtokea Kefa; tena na wale Theneshara.” (1 Wakorintho 15:3-5)

Ukiri huu wa zamani kuanzia mwishoni mwa miaka ya 30s/mwanzoni mwa 40s BK, inayoifanya iwe kati ya miaka 5-7 baada ya kusulubiwa. Nje ya Biblia pia tunayo ukiri wa Mitume unaosema kwamba:

“akateseka zamani za Pontio Pilato, alisulubiwa, akafa, akazikwa, akashuka mahali pa wafu. Siku ya tatu akafufula.”

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 02:13 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)