Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 007 (Mecca)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA KWANZA: UFAHAMU MWANZO WA UISLAMU
SURA YA KWANZA: DINI KABLA YA UISLAMU

1.5. Maka


Kipindi cha 570 Bk- hakuna patano kuhusu tarehe halisi- Muhammad alizaliwa katika mji wa Maka, mji mdogo lakini wenye kushamiri ambao ukubwa wake ni kilometa za mraba 85 na kama kilometa 50 mashariki mwa bahari ya sham bandari ya Jeda. Japokuwa hatuna taarifa sahihi zilizo huru za uhakika wa mda na wakati huu, kulingana na vyanzo vya Kiislamu vya badaye, Maka ilikuwa ni mojawapo mji wa muhimu sana ikiwa ni kitovu cha biashara kati ya kusini na na kaskazini mwa bara Arabu, Ikithibiti njia ya biashara kati ya sehemu za mashariki ya Ghuba ya Uarabuni hadi Yerusalemu na Uhajemi. Kulingana na wana historia wa Kiislamu,Wadhalimu wa Kiarabu walikuwa wakiwatoza wafanyabiashara wa Uhajemi ushuru ili kuhakikishiwa usalama wa misafara yao ya biashara. Wakati huu ndio mji huu ulikuwa ukitawaliwa na kabila ya Wakureshi. Muhammad alizaliwa katika mojawapo ya koo zinazounda kabila la Wakureshi- Wahashimu.

Maka pia ilikuwa mahali pakuu za dini za kimila za uhuhishaji katika Ghuba ya Uarabuni, Ilitumika kama mahali pa hija kwa ajili ya ibada ya miungu mingi iliyoheshimiwa na watu wa bara Arabu pamoja na madhababu za miungu mbali mbali walisafiri kwenda huko kwa nyakati nyakati tofauti za mwaka. Waarabu walikuwa wakifanya hija mara moja kwa mwaka ili watakaswe kwa machukizo ya matendo yao ya mwaka uliopita. (tendo ambalo liliendelezwa na Uislamu, japo Uislamu unadai kwamba umerithi jambo hili kutoka kwa Ibrahim). Mazingatio ya hija ilikuwa Kaaba. Kama ilivyoonyeshwa awali, Kaaba ilikuwa na muundo wa umbo la mchemraba ambayo ilijengewa jiwe jeusi na ambayo iltumika kama malaha pa kuabudia, Ingawa kuliwa na kaaba nyingi Uarabuni, hakuna ambayo ilipewa umuhimu kama iliyokuwa Maka iliyokuwepo kwa mda mrefu kabla ya kuzaliwa kwa Muhammad. Kaaba ya Maka ilizingatiwa Kipekee na takatifu; haikuruhusiwa kupanda juu yake mpaka ilazimike sana, na Wanaume huru pekee ndio walioruhusiwa, kama ililazimiaka kwa mtumwa kupnda juu yake, ilitakiwa mtumwa huyo aachiwe huru kwanza. Japo kuwa asili yake kwa hakika haijulikani,Inawezekana ilianza kutumika kwa ibada wakati ambapo mfanyabiashara tajiri wa Kiarabu alipoleta sanamu hiyo kutoka shemu ambapo kwa sasa ni kusini mwa Yordan. Mahali apoona Washirikina wakiabudu sanamu za mawe, wakiomba mvua, ushindi na kdhalika.Walimpa sanamu lililoitwa Hubal-sanamu iliyokuwa na umbo la kibinadamu iliyonakishiwa kwa kito cha madini aina ya agate nyekundu. Inasimuliwa kwamba aliiweka mbele ya Kaaba kwa ajili ya ibada ya kabila yake. Baada ya mda kila makabila mengine pia waliongeza sanamu zao na hadi wakati wa Muhammad kulikuwa na sanamu zaidi ya 300.

Cha ajabu, sio washrikina peke yao na waabudu sanamu waliofanya hija Maka kabla ya Uislamu Uarabuni, lakini pia na wayahudi na Wakristo. Kwa hakika, tunaona namna Maka ilivyoheshimika na Wakristo kwenye shairi iliyoandikwa na Ali Ibin Hatem, wakati akiwa Kiongozi wa Wakristo wa kabila la Tayy na badaye akawa swahaba wa Muhammad. Katika shairi hili, alimalaumu Kiongozi wa Wakristo waliofuata dhehebu la Unestori akisema:

“Maadui walikula njama, wasikuokoe na uovu
Ninaapa kwa Mola wa Maka na kwa Msalaba”

Hii iinaweza kushangaza na ngeni: Mkristo anamuandikia shairi Kiongozi wa Kikristo huku akiapa kwa Maka. Inashangaza pia tunagundua kwamba wakati ushindi wa kuitaka Maka, Muhammad aliamuru kila picha na sanamu ndani ya kaaba zitolewe sispikuwa alipoziba kwa mkono; aliponyanyua mkono wake, ilikuwa ni picha ya Yesu na Mariamu. Inaonyesha wazi kwamba Maka ilikuwa kituo cha ibada pia wakristo.

Ni kweli kwamba Maka ilikuwa na idadi kubwa waWakristo wenye imani za uzushi, Wengi wao wanestori waliokimbia mateso katika hima nzima ya Rumi (ambayo kwa wakati iliatawala kutoka visiwa vya Uingereza, Afrika ya Kaskazini hadi mipaka ya Uhajemi) au waliotengwa na Kanisa la Katholiki la Kilatini au kanisa la Kiothodoksi la Kiyunani. Maana Maka ilikuwa nje ya himaya ya Rumi, Konstantinpoli au Uhajemi, ilikuwa ni mahala salama kwa wanaokimbia kutoka eneo mojawapo ya hayo. Kundi hili la Wakirsto waliunga jumuiya yao iliyoitwa “Ahabish” iliitwa hivyo kutokana na jina la mlima mmojawapo ya Maka ambapo walikuwa wakikusanyika chini yake kwa ajili ibada zao. Kulikuwa pia na baadhi Wakristo watumwa.

Kwa ufupi, wakati wa kuzaliwa kwa Muhammad, Ghuba nzima na Maka hasa ilikuwa na na muunganisho wa kiibada wa ajabu baina Washirikina, Wakiristo, Wakirsto wanaofuata uzushi, na Wayahudi. Makundi haya yote yaliheshimu sana mjia wa Maka na Kaaba kwa heshima kubwa ila kwa sababu tofauti. Mfano Wayahudi walikuwatoa heshima zao hadharani kwa Kaaba ili kuwaridhisha Waarabu kwa ajili usalama wa biashara zao. Mchanganyiko huu wa kustaajabisha wa tamaduni kwa pamoja vilitengeneza mazingira ya kumpokea mtu anayemuamini Mungu mmoja akidai kwamba yeye ni mtume. Wahayudi walikuwa wakimsubiri Masihi, Wakristo nao walikuwa anasubiri ujio wa pili wa Kristo; matarajio haya yalienea na kupokelewa na jamii zingine, Kwa vile mtume kutoka Maka,Kitovu kikuu cha dini wakati huo, ilionekana ni jambo la mantiki kabisa. Na katika mazingira ndimo alimozaliwa Muhammad.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 03, 2024, at 06:19 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)