Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 046 (Do we have to?)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA NNE: FAHAMU VIKWAZO VYA KIISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA TISA: VIKWAZO VYA WAKRISTO KUSHINDA WANAPOWAINJILISHA WAISLAMU

9.1. Je tunapaswa?


Jambo moja la muhimu sana tunapoongelea jukumu ngumu na swali la umuhimu wake.Je tunapaswa Kuinjilisha Waislamu? Njia mojawapo ya kujibu swali hili ni kutazama historia ya ukombozi na sababu za Mungu kumchagua yoyote.

Wakati Mungu alipomchagua Ibrahimu, alimpa amri, akisema “Mimi ni Mungu Mwenyezi, uende mbele yangu ukawe mkamilifu” (Mwanzo 17:1) Alipowachagua Waisrael, Alisema “Nanyi Mtakuwa kwangu ufalme wa makuhani, na taifa takatifu. Haya ndio maneno utakayo waambia wana wa Israel (Kutoka 19:6). Hivyo sababu ya kumchagua Ibrahimu ni ili Ibrahimu atembee mbele za Mungu, na kutembea mbele za Mungu kunahitaji kuwambia mataifa juu yake. Israel ilichaguliwa kuwa taifa ufalme wa makuhani. Kuhani ni yule anayewambia watu juu ya Mungu na kuwafundisha anachokisema Mungu.

Mungu alipomuita yoyote katika Agano la Kale, hakuwaita ili kuwapendelea badala yake ilikuwa ni uchaguzi kwa ajili kazi yake. Kwa maneno mengine, Mungu hakuchagua yoyote kwa sababu walikuwa bora au wacha Mungu kuliko yoyote, lakini kwa sababu aliwateua wao kwa ajili ya kazi. Walichaguliwa kutangaza kwa mataifa yote kwamba Mungu anatawala. (Zaburi 96:10)

Namna hiyo hiyo, katika Agano la Jipya, hii ndio iliyokuwa amri ya mwisho ya Kiristo:

“Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani. Basi enendeni,mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi,mkiwabatiza kwa Jina la baba na la Mwana na Roho Mtakatifu, na kuwafundisha kuyashika yote niliyowamuru ninyi na tazama mie nipo pamoja nanyi siku zote nanyi hata ukamilifu wa dahari” ( Mathayo 28:18-20)

Amri hii kwa namna yoyote haiwezi kukwepwa au kuelezwa mbali tu. “Mataifa yote”inamaanisha hivyo tu, Yote bila ubaguzi, na bila shaka Waislamu wamejumuishwa pia kwenye neno “Wote”.

Kabla ya Kristo kupaa, aliwambia wanafunzi wake

“…. Mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu, nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi” (Matendo 1:8)

Kuna hatua moja muhimu sana ya kuzingatia hapa kwenye aya hii. Amri ya Kristo ya kuwa mashahidi wake inaanzia Yerusalemu. Hii mara nyingi imeeleweka kumaanisha kwamba tunatakiwa kuanza na watu walio karibu na sisi na kisha kundelea mbele zaidi ya hapo. Hata hivyo, tafisri ya namna hiyo inapuuza kwamba hakuna Mtume yoyote wa Yesu aliyekuwa anatokea Yerusalemu lakini badala yake walikuwa wakitokea Galilaya. Kwao, Yerusalemu ndio iliyokuwa sehemu ngumu kwenda na kutangaza Injili. Ilikuwa kitovu cha dini na mamlaka ya kisiasa. Kutanganza Injili Yerusalemu kwa wakati huo ilikuwa ni kazi ya hatari sana, maana hiyo ingemaanisha kwenda kinyume na mamlaka ya Rumi, kinyume na mamlaka Kiyahudi pia wakati huo huo. Hivyo mmoja kama angeweza kuhubiri Injili Yerusalemu, basi kuhubiri Injili sehemu zingine za dunia ingekuwa jambo la rahisi kwake.

Kanisa la kwanza walielewa jukumu hili kwa uwazi kabisa. Petro alihubiri kwamba “Enyi watu wa Uyahudi, na ninyi nyote mkaao Yerusalemu” (Matendo 2:14b). Kanisa lililazimishwa kuongea kile walichokiona na kukisikia, hata kama ingawa walijua wangeadhibiwa kwa kufanya hivyo ( Matendo 4:20-29). Kwa wakati huo kuhubiri Injili ilikuwa ni kosa la jinai lenye kuadhibiwa, ambayo ingekuwa- na kwa kweli wakati mwingine adhabu yake ilikuwa ni kifo, maana kuhubiri ilikuwa ilichukuliwa kama kufuru (Kwa mtazamo wa Kiyahudi) au uhaini ( Kwa Mtazamo wa Himaya ya Rumi). Kuna ushahidi mwingi kutoka kwenye Biblia unaoelezea umuhimu wa kazi ambayo tunaweza na mda zaidi nao, Lakini ni wazi lakini naamini hoja iko wazi kwenye Biblia nzima. Tunapaswa kuwambia watu wote juu ya Kristo, bila kujali hatari ya kufanya hivyo, au ugumu wake.

Hivyo baada kuweka imara hoja hii kwamba ni kitu tunacholazimika kufanya, kwa nini Wakristo wachache wanashughulika na kuinjilisha Waislamu? Kinachokwamisha njia yao ni nini-na muhimu zaidi- hicho kinachokwamisha tunaweza kutokukiruhusu kutuzuia? Sehemu iliyobaki ya sura hii, tutaangazia baadhi ya sababu nyingi hizo zinazotufanya tuone aibu na kuacha kutekeleza amari hii.

Kichokwamisha njia, na namna gani tunaweza kutokuruhusu kituzuie?

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 10:23 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)