Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 064 (CHAPTER ELEVEN: ADVICE FOR ENGAGING IN THEOLOGICAL DISCUSSIONS WITH MUSLIMS)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA NNE: FAHAMU VIKWAZO VYA KIISLAMU DHIDI YA INJILI

SURA YA KUMI NA MOJA: USHAURI WA KUSHIRIKISHA MIJADALA YA KITHEOLOJIA NA WAISLAMU


Kabla hatujajadili Vizuizi vvya Waislamu juu ya Mafundisho ya Biblia. Nataka tutazame baadhi ya vitu vya jumla vya kufanya na kutokufanya kwa Wakristo ambao wanashirikisha mijadala ya Kitheolojia na wasilamu. Wakristo hawatakiwi kulenga ubishi ili kuthibitisha kwamba wana majibu kwao. Lakini pia hawatakiwi wakija juu huku hawajibu maswali na wakijaribu kubadilisha mada. Kwa sababu hii itawapa Waislamu mawazo kwamba maswali yao mengine haya majibu. Njia ya Kibiblia ya kujadiliana na wasio Wakristo imetolewa kwetu katika Matendo 17 na 25. Hapa tuna namna ambavyo Mtume Paulo alivyoshughulika na Mpinzani wake, Hakukwepa swali lakini alijibu kwa heshima huku bado moja kwa moja bila kukwepa wala kupunguza ukweli wa imani na kila mara kurejesha hoja iwe ni Kristo. Hapa ni baadhi ya mambo machache tunapswa kuyakumbuka kwenye mjadala.

  1. Lengo lako sio kushinda ubishi wa Kitheolojia; badala yake ni kumuongoza mwingine kwa Kristo. Jitahidi kwa kadri unavyoweza kuondoa vikwazo kati yako na mtu unayewaliana naye bila kungojea matokeo. Kumshawishi mtu kuamua sio kazi yako, ni kazi ya Roho Mtakatifu. Hatujui namna Mungu anavyotumia mazungumzo yetu. Ni kweli kwamba “Katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti: Na katika wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima” (2 Wakorintho 2:16). Mhimize unayeongea naye kusoma Biblia kama swali imejibiwa, Kwa sababu ina nguvu ya kushawishi kuliko maneno yako.
  2. Zuia mazungumzo yabaki kwenye mada moja au mbili. Pale inapowezekana, jaribu kuanzisha mada hizo kabla. Mara ya kwanza Unayewasiliana naye atakuwa akirukia rukia mada mpya kabla ya kufikia hitimisho ya mada iliyoko, waambie wachukue mada hiyo mpya ili kuijadili mkimaliza iliyoko. Kurukia mada moja kwenda nyingine inaweza kuwa ni njia sahihi ya kupata majibu, lakini pia ni ujanja unaotumika na wengi wasioamini kukwepa hoja mahali wanapoona wanatakiwa kufanya maamuzi. Pia ni kupoteza juhudi kwenu wote.
  3. Kama ukiulizwa juu ya kitu fulani usichokijua, wewe sema tu kwamba haujui. Usijaribu kujitungia majibu, Lakini badala yake mwambie unayeongea naye kwamba utafanya utafiti kuhusu mada husika na kuwarejea. Kuwa makini usiache kurudi kwao, kwa sababu hiyo itakuwa na matokeo hasi sana kwao na inaweza kuzingatiwa kama kutokuwa na heshima au kukwepa.
  4. Haijalishi una adabu na muangalifu namna gani karibuni au baadaye utakanyaga vidole vya miguu ya mwingine. Kwa Waislamu, haijalishi unaonyesha adabu kiasi gani bado watahitaji kuheshimiwa zaidi. Katika mazungumzo namna hiyo kuwa mkweli na mpole ni muhimu na yana matokeo makubwa sana kwa unayeongea naye, lakini kumbuka ifanyike bila kupunguza ukweli wa theolojia. Nakumbuka niliwahi kukutana na Mmarekani aliyejiunga na Uislamu. Tukajikuta tunaongelea dini, katika mojawapo ya maongezi, akatumia tafsiri isiyo sahihi ya aya ya Qur’an, Nikajaribu kwa upole kumuonyesha tafsiri nyingine sahihi ambayo iko karibu zaidi ya Kiarabu, ingawa mpinzani wangu hajui neno lolote la Kiarabu na japokuwa Kiarabu ni lugha yangu mama, alikasirika na kuondoka. Baadaye jioni nikapigiwa simu na mwenyeji wetu kuomba msamaha kwa ajili ya tabia ya rafiki yake. Niliambiwa kwamba waliokuwepo pale walikerwa na tabia na muelekeo wa Muislamu wakasema aliondoka kwa sababu hoja zake zilikuwa dhaifu na alihangaishwa na kutokuweza kwake kujibu maswali. Hoja yangu ni kwamba upole na uimara wa hoja saa zingine hautakuwa na matokeo kwa unayeongea naye, itakuwa na matokeo makubwa sana kwa wanaowasikiliza na badaye inaweza kuwa na matokeo kwake. Unaweza kushinda mashambulizi ya mpinzani wako kwa kuonyesha heshima kuliko upinzani. Saa zingine ni vizuri kuwambia watu unaongea kwamba unatarajia kutendewa kwa namna unavyowatendea. Inaweza kukusaidia binafsi kujua kwamba haujadiliani kwa ajili yako binafsi lakini unajaribu kuwasaidia waokolewe. Haujadiliani nao tu lakini kuna vita vya kiroho vinaendelea katika uwanja wa mapambano.
  5. Weka akilini kwamba wakati mwingine mpinzani wako anaweza kujaribu kukufanya ukasirike au uje juu kwa malengo, ama kujithibitishia kwamba hauwezi kujibu mapingamizi yao au kujenga hoja kwa yoyote anayesikiliza kwamba hauna majibu na ndio maana unakuwa na hasira. Wataenda mbali kuomba masamaha kama wamekukera kwa maswali yao, Hivyo kuwa juu kwenye mjadala, tena, kumbuka sio suala kujivuna kwako “Wakati mwingine unatakiwa kushindwa hoja lakini kumuokoa mtu.”
  6. Hakikisha unaonyesha wazi kwa unayeongea naye umuhimu wa mada. Hii ni muhimu sana kwa maisha yake kwa sababu inahusu uzima wake wa milele. Hiyo inamaanisha lazima uipe mada umuhimu mkubwa. Kama usipofanya, unaweza kutarajia mpinzani wako afanye? Na kama uko makini na mada na wewe watakuchukulia kwa umakini.
  7. Jaribu sana kukwepa kuingia kwenye mjadala wa maswali kama “Unafikiria nini juu ya Muhammad?” au “Unafikiri nini juu ya Qur’an”? Ni rahisi sana maswali haya kusababisha ugomvi, au kwa bahati sana kusababisha mazungumzo kutokuendelea. Jibu kwa ufupi sana kwa usahihi, kama vile “ Hauitaji mawazo yangu kuhusu Muhammad au Qur’an au Tulikuwa tunaongelea Kristo sio Muhammad, na kama ukisoma Bilia unaweza kujipatia mtazamo wako mwenyewe” Jaribu kuwa sahihi bila Kumshambulia Muhammad kwa sababu haitaisha kwa usalama.
  8. Mazungumzo yoyote juu ya Muhammad yanatakiwa kufanywa kwa uangalifu mkubwa. Waislamu wanaweza kupinga bila hasira mtu anayesema hamuamini Mungu, Lakini watajibu kwa hasira nyingi mtu yoyote anayemfanya Muhammad kuwa duni. Bila shaka kama wakristo hatuwezi kumtukuza Muhammad lakini pia kwa wakati huo huo hatupaswi kumkashifu. Unaweza kujaribiwa kuongelea tabia za maadili ya Muhammad, lakini kuepuka hilo. Kwanza hii haitasaidia sana, Utajikuta unaingia kwenye maongezi ya nani ana maadili mazuri zaidi kati ya Muhammad na Manabii wa Biblia. Kama Waristo tunavyoamini kwamba kila mwanadamu ni mwenye dhambi, kuthibitidha kwamba Muhammad ni mdhambi haitasaidia sana. Hata hivyo ukiongea kwa mukhtasari nafsi ya Kirsto na ulinganifu wa Muhammad na Kristo unaenda kutokea moja moja kwenye akili ya Muislamu bila kukuhitaji kutaja. Nakumbuka miaka iliyopita kulikuwa harusi kanisani kwetu, Baba wa bibi harusi alikuwa akifanya kazi katika mojawapo ya taasisi kubwa za Kiislamu hivyo akaalika Waislamu wengi anaofanya kazi nao kuja. Mchungaji wetu hakuwa na maneno mengi katika mahubiri ukumbi ambao umejaa Waislamu. Alianza kwa kuongelea harusi ya Kana, namna ambavyo Kristo hakukataa au kuondoka aliombwa kufanya muujiza, akaendelea kuongea namna ambavyo Kristo alikuwa tayari kusaidia wenye shida, kujibu maswali yao. Hata kujibu mashutumu na lawama zao. Hakusema neno juu ya Muhammad au Uislamu lakini Waislamu katika ukumbi ule walishaanza kulinganisha kati ya Kristo na Muhammad hasa alivyokataa kufanya muujiza alipoombwa, alivyokataa kusaidia mwenye shida na namna alivyokuwa akikasirika kwa waliomkosoa, kukataa kujibu maswali na kuwakatisha tamaa wafuasi wake wasiwe wanauliza uliza maswali. Hawakuweza kumkasirikia mchungaji maana hakuna alilosema juu ya Muhammad lakini walishindwa kujizuia kulinganisha baina ya wawili.
  9. Chukua tahadhari zaidi unapotumia maneno ya Kitheolojia kwa sababu:
    a) ni mara chache sana humaniisha kitu kile kile kwa Wakristo na Waislamu;
    b) wakati mwingine maneno tunayotumia yanaweza kutomaanisha chochote kwa Waislamu kama vile Ufalme wa mbinguni,utakatifu, Mpakwa mafuta na dhalika; na
    c) wakati mwingineni maneno au istilai tunazotumia yanaweza hata kuchukuliwa kama kufuru kwa Muislamu, kwa mfano wana wa Mungu, Ndugu wa Mungu, damu ya Mungu na kadhalika. Tunatakiwa kujua kwamba maneno hayo kwa Muislamu yanamaanisha nini na kuweza kuyafafanua tulimaanisha nini tulipoyatumia Tunatakiwa kutumia maneno yanayoeleweka- tena bila kupunguza maana ya imani. Kwa mfano ni rahisi kuongea habari za Kristo na Muislamu kwa kutumia neno “Kristo” na sio Jina la Yesu maana wao wanajua “Isa” tu basi kama nabii na sio Yesu Mwana wa Mungu, na bila shaka hatuna shida kumuita Yesu kama Kristo.
  10. Kila mara unapoinukuu Biblia jitahidi kufaya hivyo kutoka kwenye Biblia na sio kwenye kukariri, mara nyingi itafanya unachokisoma kiwe wazi, na utamfanya unayeongea naye aweze kurejea Biblia na kusoma Biblia na kuelewa maana hasa ya maudhui ya aya yenyewe.
    Hata hivyo unapoisoma Biblia kuwa mwangalifu namna unavyoichukulia, Kama Wakristo hatuheshimu karatasi iliyoandikwa biblia humo na kuchapwa, mara nyingi tunachora, Biiblia zetu, kuandika jumbe kadhaa na kuweka alama na kadhalika. Haya yote hayakubaliki kwa Muislamu ambaye anaipa hadhi kuu sana Qur’an na hawezi kuota kuichora na kuiwekea alama Qur’an. Hivyo itasaidia sana kuwa na nakala ya Biblia ambayo ndani yake hakuna maandishi yako au alama ndani yake, Hivyo hivyo unapomaliza kuisoma Biblia yako usiiweke chini bali iweke juu ya meza au juu ya kiti. Hili linaweza kuonekana halina umuhimu kwetu, lakini kwa Muislamu ina umhimu mkubwa sana maana inaweza kumpa tafsiri kwamba tabia yako haiheshimu maandiko matakatifu.
    Hivyo kama unayo Qur’an na unataka kutaja aya ndani yake kama rejea, epuka kutumia yako, na angalia kama unaoongea nao wanazo zao ili kuwaomba wazitumie, waombe watafute kwa ajili yako- Baadhi ya Waislamu- kwa kulingana na mafundisho ya Muhammad wanaamini kwamba wasio- Waislamu hawatakiwi kugusa Qur’an. Bila shaka uwepo wa Qur’an kwenye mitandao imefanya kuwa rahisi kutafuta aya kwenye mtandao na kujisomea – na baadhi ya Waislamu hawana shida nayo.
  11. Kabla ya majadiliano unapaswa kujua sio kila kitu ambacho Qur’an inakubalina na Biblia lakini kuna mambo ambayo hazikubaliani. Maeneo zinapokubaliana bila shaka ni muhimu sana kuliko mada ambazo hazikubaliani, bila shaka kufanana huko hakuna maana yoyote katika Uislamu wala hayawezi kueleweka isipokuwa kupitia lenzi ya Biblia. (Aangalia Sura ya 12 chini)
    Tunatakiwa pia kujua tunachokiamini, kwa sababu wakati mwingine tunaweza kuingia katika mjadala usio na maana ambayo haina athari yoyote ya Kitheolojia kivyovyote, mfano mda unaoweza kutumia kutetea dhambi za mtu ( hata zako wewe mwenyewe). Tumekwisha kuamini kwamba kila mmoja wetu ni mdhambi (Warumi 3), hivyo hakuna haja ya kuhalalisha kitu ambacho papa au padre amefanya.
  12. Kubali mambo unayokubaliana nayo—kwa wakati huo- na kisha jenga katika hayo. Qur’an ina vijisehemu vya hadith nyingi sana za Biblia na nadharia lakini bila taarifa na mafafanuzi kamili, wakati Biblia inaelezea hivi vitu kwa undani sana na kwa ufasaha. Kulenga vitu hivi vinaweza kumfanya mkristo kuwa huru kuongelea Biblia, maana unayeongea naye anaweza kuvutiwa kile wanachosema Wakristo kuhusu kitu hicho hicho alichokisoma kwenye Qur’an kama vile Kuzaliwa kwa Kristo, Kutoka, Miujiza ya Yesu na Musa na kadhalika. Angalia sura inayofuata kwa mjadala wa vitu hivyo.
  13. Kila mara jali mtazamo wa unayeongea naye, fikiria kanuni ya dhahabu “Chochote unachotaka kutendewa, watendee wengine, maana hii ndio Torati na manabii” (Mathayo 7:12) Kama ungekuwa kwenye nafasi zao, ungetaka kutendewaje? Ni vizuri siku zote kwamba umpe taarifa zote sahihi halafu uwaache kufanya maamuzi; usiamue kwa ajili yao. Ni rahisi kwa watu kubadilisha nia zao wanapofikiri kwamba walifanya wenyewe kuliko wakidhani kwamba uliwalazimisha cha kufikiri.
  14. Weka akilini ni dhehebu gani, au kikundi, ya Muislamu unayeongea naye. Kama unaongea na Msuni mhafidhuna, hiyo inaweza kuwa rahisi kukubaliana na kitu unachonukuu kutoka kwenye Qur’an au Hadith kwa sababu wamevizoea, lakini inaweza kuwa ngumu kwao kuwafanya wasome Biblia. Kama unaongea na Muislamu wa jina tu, hiyo ina umuhimu mdogo sana wa kunukuu Hadith au Qur’an, maana inawezekana hawajahi kuvisoma.
  15. Mwisho, kama Mtumwa wa Kristo, kumbuka ushauri wa mwanatheolojia wa karine ya 18 wa Ujerumani Johann Albrecht Bengel: “Usiingie kwenye mjadala bila ufahamu, bila upendo, na bila sababu.” Kwa hili naweza kuongeza tu "bila maombi".

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 10, 2024, at 01:23 PM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)