Home
Links
Contact
About us
Impressum
Site Map?


Afrikaans
عربي
বাংলা
Dan (Mande)
Bahasa Indones.
Cebuano
Deutsch
English-1
English-2
Español
Français
Hausa/هَوُسَا
עברית
हिन्दी
Igbo
ქართული
Kirundi
Kiswahili
മലയാളം
O‘zbek
Peul
Português
Русский
Soomaaliga
தமிழ்
తెలుగు
Türkçe
Twi
Українська
اردو
Yorùbá
中文



Home (Old)
Content (Old)


Indonesian (Old)
English (Old)
German (Old)
Russian (Old)\\

Home -- Kiswahili -- 17-Understanding Islam -- 081 (The Bible Says the Spirit is God)
This page in: -- Arabic? -- Bengali -- Cebuano? -- English -- French -- Hausa -- Hindi -- Igbo -- Indonesian -- KISWAHILI -- Malayalam -- Russian -- Somali? -- Ukrainian? -- Yoruba?

Previous Chapter -- Next Chapter

17. Ufahamu Uislamu
SEHEMU YA TANO: FAHAMU MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA INJILI
SURA YA KUMI NA TATU: MAPINGAMIZI YA WAISLAMU DHIDI YA UKRISTO
13.3. Mapingamizi juu ya Utatu

13.3.3. Biblia inasema Roho ni Mungu


  • “Petro akasema, Anania, kwa nini shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? ilikuwaje hata ukawaza neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.” (Matendo 5:4)
  • “Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake.” ( Warumi 8:9)
  • “Lakini ajapo huyo Msaidizi, nitakayewapelekea kutoka kwa Baba, huyo Roho wa kweli atokaye kwa Baba-yeye atanishuhudia.” (Yohana 15:26)
  • “Basi “Bwana” ndiye Roho; Walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru.” (2 Wakorintho 3:17)

Agano la kale linamuongelea Mungu katika uwingi mahali pengi sana. Kwanza katika Mwanzo 1:26 Mungu anajiongelea akitumia uwingi Elohim kwa kitenzi cha uwingi wa kuwasiliana; katika Mwanzo 11:6-7 anatumia umoja wa Yahweh kujiita binafsi lakini anatumia uwingi; na katika Isaya 6:8 anatumia umoja na uwingi kwa pamoja anaposema “Na nimtume nani, na nani atakayenda kwa ajili yetu?” Aya ziko wazi kwamba hatuongelei moja kamili lakini umoja katika moja. Waislamu wakati wanapojaribu kusema kwamba uwingi wa “sisi” unamaanisha uwingi wa Kifalme (Ufalme unaotumia “sisi”) kama inavyotumika katika Qur’an. Hiyo ingekuwa halali kama Biblia ingeandikwa kwa Kiarabu lakini haikuwa; Kiebrania hakina uwingi wa Kifalme. Kuna aya zingine pia katika Biblia zinazofanya uwezekano huo wa uwingi wa Kifalme usiweze kufanya kazi, kama vile katika Isaya 48:16:

“Nikaribieni,Sikieni haya,tokea mwanzo sikunena kwa siri, tangu yalipokuwepo, Mimi nipo na sasa Bwana Mungu amenituma na roho yake.”

Aya hii kwa wazi inaonyesha kwamba Mungu, Muongeaji, ni wote anayetuma na aliyetumwa.

Zaidi ya hapo Biblia haiishii kwenye maneno tu lakini inaweka wazi Uungu wa Yesu kupitia matendo. Katika Injili ya Mathayo Yesu alipobatizwa, punde akatoka majini, na tazama, mbingu zikafunguka juu yake, na akaona Roho wa Mungu akija kama njia juu yake na tazama, sauti ikatoka mbinguni ikisema,

“Huyu ni Mwanangu, Mpendwa wangu, ninayependezwa naye” (Mathayo 3:16-17).

Hapa tunaona Kristo ndani ya maji, Roho Mtakatifu akionekana kama njia na sauti kutoka mbinguni.

Baraka iliyotolewa kwa kanisa la Korintho pia inaonekana kutaja watatu walio moja:

“Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na pendo la Mungu, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nanyi nyote.” (2 Wakorintho 13:14)

Mwisho, Kipengele kinachohusu utatu katika tabia ya Mungu ni jambo ambalo Muislamu kwa uchache sana kama hata amewahi kuipa uzito. Qur’an inawaambia Waislamu kufikiria juu ya uumbaji wa Allah (Qur’an 7:158; 33:20; 30:8; 86:5; 2:259), Lakini inawakatisha tama- na baadhi ya wanazuoni wanaona kwamba ni jambo lililopigwa marufuku kabisa- kufikiria juu ya tabia ya Allah. Hadith inayotoka kwa Muhammad inasema:

“Fikiria kuhusu uumbaji wa Allah na usiwaze juu ya asili yake na kiini yake, usije ukapotea (al-Laka’y, Taasisi ya imani).

Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wameenda mbali zaidi. Haya ni mfano wa yale waliyoyasema:

“Awaye yote anayemuwaza Allah na tabia zake atapotea, na yoyote anayefikiria uumbaji wa Allah na ishara zake anazidisha imani yake.” (al-Asbahani, al-Hijja)
“Ni wajibu wa kila Muislamu kuamini yote ambayo Allah amejielezea na kuacha kufikiri juu ya Allah” (Naeem ibn Hamad, Al-Laka’y, Taasisi ya Imani)
“Imeharamishwa kufikiri kuhusu kiini cha Allah kwa sababu wanadamu wanapaswa kufikiria tu yale wanayoyajua, na Allah anapita uelewa wote.” (al-Sanany, al-Taneer)

Mawazo kama hayo juu ya Mungu yanawazuia Waislamu kufikiri kuhusu kiini cha Mungu, na tunapaswa kuwasaidia kushinda hilo. Tunakubaliana na Waislamu kwamba Mungu anapenda, anatoa, anaongea na anasikiliza.Tabia hizi wakati wote zimekuwa zikifanya kazi; hakuna wakati ambapo Mungu alikuwa hapendi, hasikilizi, haongei au hatoi. Swali linaloinuka ni: Kabla ya uumbaji wowote ule hizi tabia zilikuwa zinafanyaje kazi? Kama Mungu alijipenda mwenyewe, alijipa mwenyewe, alijiongelesha mwenyewe, na akajisikiliza mwenyewe, basi tabia zote zisingekuwa kamili na zingegeuka kitu tofauti. Au kama zilikuwa hazifanyi kazi mpaka uumbaji, hiyo ina maana Mungu anahitaji uumbaji wake ili kujaza utupu wake mwenyewe ili kuelezea Umilele wake, na tabia zake za Kiungu.

Wanazuoni wa Kiislamu waliona shida walipojaribu kuchukua dhana ya moja kamili ya Mungu katika theolojia ya Kiislamu. Wakaishia na tamko kama:

“Katika mambo hayo hakuna kanusho au uthibitisho umeelezwa, mambo ambayo watu wamepingana kama vile mwili wa Allah, au kuwa katika eneo fulani au nafasi na kadhalika. ; Ahlu-s‐Sunnah ( Waislamu wa Suni) wanazuia kuongelea juu yake. Hawathibitishi au hawakanushi mambo haya kwa sababu ya ukweli kwamba hakuna kilichokuja kwetu tukakifahamu kuhusiana nayo” (Maelezo mafupi ya al-‘Aqeedatu al-Hamawiyyah).

Taarifa kama hiyo ni kama askari wa nje tu; inatumika kukwepa mazungumzo yoyote yale maana Qur’an inaelezea tabia za kibinadamu za Allah kama vile mkono (Qur’an 48:10), uso (Qur’an 28:88), upande (Qur’an 38: 55-56). Hadith pia inasema Allah ana mguu:

“Moto wa kuzimu utaendelea kusema “Bado kuna wengine (watu wa kuingia) Mpaka Bwana wa nguvu na heshima atakapoweka mguu wake juu yake na itasema ‘Qat! Qat! (Inatosha, inatosha!).” (Sahih Bukhari)

Kama tukichukulia masharti ambayo Wanazuoni wa Kiislamu wanaweka wanapomuongelea Allah, hatutakuwa na uwezo wa kumuongelea kabisa. Tunatakiwa kuthibitisha tabia zake zote bila kuzikanusha, kubadilisha maneno yake, kuzikataa, kuzifananisha na chochote kile, kuzichora kwa kuzilinganisha, kupotoa kutoka katika hizo sifa, au Kuziita kwa mfano na kadhalika. Kutokuweza kwetu kuongelea Mungu katika mazingira hayo ni kwa sababu eti tunaweza tu kufahamu lugha ya dhana inayotambulika na wanadamu tu. Hivyo Qur’an inaposema Allah ana mikono miwili, uso, macho mawili, vidole, goti na miguu, hayo yanatakiwa kufahamika kama ambavyo maneno hayo yanavyomaanisha sio kinyume chake, kwa sababu hiyo haiwezi kupatanishwa na Uislamu kukanusha Mungu kutwaa utu, basi Waislamu wamekatazwa kuyaongelea kabisa. Tatizo kama hilo haliwasumbui wakristo kwa sababu sifa na tabia za Mungu zinafanya kazi katika utatu. Hakubadilika baada uumbaji, hahitaji uumbaji kumtafsiri alivyo; sifa zake hazikuanza kufanya kazi punde baada uumbaji. Baba alimpenda mwana kabla ya Uumbaji, na walimpenda Roho wote kwa pamoja. Kama tunavyoona Uislamu haukatai dhana ya utatu wa Ukirsto (Wameelewa vibaya kile tunachkiamini), Na zaidi, Fundisho la Kikristo ya utatu ndio suluhisho kwa matatizo yaliyotengenezwa na Uislamu ya dhana ya Moja kamili.

Kwa kufupisha:

  • Wakristo wanaamini katika Umoja katika moja sio moja wa utatu.
  • Utatu wa Kikrsto hauna mke au mtoto wa kuzaa.
  • Wakristo hawajawahi kumfanya mwanadamu kuwa Mungu.
  • Uislamu haupingi Utatu halisi wa Kikristo, badala unapinga fundisho la uwongo ya utatu ambayo Wakristo hawajawahi kusema kuuamini.
  • Utatu wa Kikristo haumshirikishi yoyote pamoja na Mungu, badala yake unafafanua namna Mungu alivyojifunua mwenyewe.
  • Waislamu hawawezi kujadili asili na kiini cha Allah maana imekatazwa kwao na Wanazuoni.
  • Sababu pekee ya Waislamu kukataa utatu ni kwa sababu wanafikiri ni aina fulani ya ushirikina.

www.Grace-and-Truth.net

Page last modified on March 11, 2024, at 02:04 AM | powered by PmWiki (pmwiki-2.3.3)